"Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana."
Waefeso 2:21.
Kupitia kwa neema ya Kristo utafanya jitihada za makusudi ili ushinde dharau yote, ukatili, ukali, njia zote za mienendo isiyofaa na kutokuwa na adabu….
Kisu kikubwa cha ile kweli kimekutoa toka kwenye machimbo ya dunia. Ninyi mlikuwa mawe yenye mikwaruzo yaliyokuwa na kona zenye ncha, yakiwakwaruza na kuharibu yeyote uliyekutana naye; ipo kazi ya kufanya ili kulainisha kona hizi zinazoparuza. Kama unatambua thamani ya kazi ambayo sharti ifanywe kwenye karakana ya Mungu, utaruhusu mapigo ya shoka na nyundo. Kujiheshimu kwako kutaumizwa, hadhi unayojifikiria mwenyewe itakatiliwa mbali na shoka na nyundo na mkwaruzo wa tabia yako utalainishwa na wakati hulka ya nafsi na ya kimwili vikishughulikiwa, ndipo jiwe litakapopata uwiano unaotakiwa kwa ajili ya jengo la kimbingu na ndipo ulainishaji, usafishaji, uondoaji wa utata, mchakato wa uboreshaji utakapoanza. Nawe utaumbwa kulingana na muundo wa tabia ya Kristo. Sura yake mwenyewe inafaa iakisiwe kwenye tabia iliyong’azwa ya mwanadamu na jiwe litafanywa lifae kwa ajili ya jengo la kimbingu….
Ikiwa sisi siyo wanaume na wanawake walio bora zaidi, ikiwa sisi hatuna mioyo yenye wema zaidi, yenye huruma zaidi, yenye staha zaidi, iliyojawa na wema zaidi na upendo zaidi; ikiwa sisi hatuwadhihirishii wengine upendo ambao ulimleta Yesu duniani katika utume wake wa rehema, hatuwi mashahidi wa uweza wa Yesu Kristo duniani. Yesu hakuishi ili kujifurahisha mwenyewe…. Alikuja ili ainue, aadilishe, awape raha wale wote aliokutana nao… Kamwe hakufanya kitendo cha kikatili, wala kamwe hakusema neno lisilo na adabu.
Ni fursa ya pekee kwa ajili ya kila kijana kuwa kiumbe kizuri kulingana na tabia yake…. Mtafute Bwana kwa dhati zaidi, ili upate kusafishwa zaidi na zaidi, uwe umeelimishwa zaidi kiroho.

EmoticonEmoticon