YUSUFU MKRISTO MWUNGWANA




Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
Mwanzo 39:21.

Yusufu aliona kuuzwa kwake Misri kama janga kubwa zaidi ya yote ambayo yangeweza kumpata; lakini aliona umuhimu wa kumtumainia Mungu kuliko wakati wowote mwingine alipokuwa chini ya ulinzi wa upendo wa baba yake. Yusufu alikuja na Mungu pamoja naye hadi Misri na ukweli huu ulidhihirishwa kwa mwenendo wake wenye uchangamfu katikati ya huzuni yake. Kama sanduku la Mungu lilivyoleta raha na mafanikio kwa Israeli, ndivyo huyu kijana aliyempenda Mungu, aliyemcha Mungu alivyoleta baraka Misri. Hili lilidhihirika kwa namna iliyokuwa wazi kabisa kiasi kwamba Potifa, mwenye nyumba ambapo alitumika, aliona kuwa mtumwa aliyemnunua alikuwa ndiye sababu ya baraka zake zote.

Dini ya Yusufu ilifanya tabia yake iwe nzuri na huruma zake kwa binadamu kuwa hai na thabiti, licha ya majaribu yake yote. Wapo wale ambao wanapojisikia kwamba hawakutumiwa vyema, wanakuwa wakali, wasio na shukrani, wepesi kughadhibika na wasio na adabu kwa maneno na mwenendo wao. Wanajishusha katika hali ya kukata tamaa, huku wakichukiza na kuchukia wengine. Lakini Yusufu alikuwa Mkristo. Mara alipoingia kwenye maisha ya gereza, alileta uangavu wa kanuni zake za Kikristo na kuzitumia; akaanza kuwa wa manufaa kwa wengine. Akaingia kwenye taabu za wafungwa wenzake. Akawa mchangamfu, kwani alikuwa Mkristo muungwana. Mungu alikuwa anamuandaa kupitia kwenye somo hili kwa ajili ya mazingira ya wajibu, heshima na manufaa makubwa naye alikuwa tayari kujifunza; kwa wema aliingia kwenye masomo ambayo Bwana alikuwa amfundishe. Alijifunza kuchukua nira wakati wa ujana wake. Alijifunza kutawala kwa kujifunza unyenyekevu yeye mwenyewe kwanza….

🏾Sehemu ambayo Yusufu aliipitia ikiunganishwa na sehemu za gereza lenye giza, ndiyo ambayo hatimaye ilimuinua hadi kufikia mafanikio na heshima. Mungu alikusudia kwamba apate uzoefu kupitia kwa majaribu, shida na taabu, ili kumuandaa kujaza nafasi ya heshima ya juu. Yusufu alikwenda na dini yake kila mahali na hii ndiyo iliyokuwa siri ya uadilifu wake ambao haukuyumba.
Image may contain: text, outdoor and nature
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.