JIHADHARI KUFANYA USHIRIKA NA ULIMWENGU



(Ufunuo 18:1-3 imenukuliwa) Wakati ujumbe huu unapotolewa, wakati utangazwaji wa ukweli unafanya kazi yake ya kutenganisha, sisi kama askari wa Mungu waaminifu hatuna budi kutambua ni nini nafasi yetu hasa. Hatupaswi kuungana na watu wa ulimwengu, ili tusije tukajazwa kwa roho yao, ili utambuzi wetu wa kiroho usije ukachanganyikiwa na kuwatazama wale wenye ukweli na wanaotoa ujumbe wa Bwana kwa mtazamo wa makanisa yanayokiri kufuata Ukristo. Wakati huo huo hatupaswi kuwa kama Mafarisayo na kujitenga mbali nao. - EGW' 88 1161 (1893).

Wale wanaokesha na kungoja kwa ajili ya kutokea kwa Kristo ktk mawingu ya mbinguni hawatakuwa wakijichanganya na ulimwengu ktk vikundi na mikusanyiko ya starehe kwa ajili tu ya maburudisho yao. - Ms 4, 1898.

Kujifunga sisi wenyewe kwa mikataba au ktk kufanya ubia au ushirikiano wa kibiashara pamoja na wale wasio wa imani yetu hakupo ktk utaratibu wa Mungu. - RH Aug. 4, 1904.

Tunapaswa kuungana na watu wengine kwa kiwango kile tunachoweza na bila kukiuka kanuni. Hii haimaanishi kuwa tunapaswa Kushirikiana nao ktk nyumba za vyama na vikundi vyao, lakini tunatakiwa kuwajulisha kuwa tunazingatia na kujali zaidi suala la kiasi. - Te 220 (1884).
Image may contain: cloud, sky and text

Previous
Next Post »
Powered by Blogger.