Wakati Kristo alipoingia ktk patakatifu pa patakatifu pa hekalu la mbinguni ili kutekeleza kazi ya mwisho ya upatanisho, aliwakabidhi watumishi wake ujumbe wa mwisho wa rehema unaopasa kutolewa kwa ulimwengu. Huu ni ujumbe wa onyo wa malaika wa tatu wa Ufunuo 14. Nabii anaona kuwa mara tu baada ya kutangazwa kwake, Mwana wa Adamu atakuja kwa utukufu ili kuvuna mavuno ya ulimwengu.
Onyo la kuogofya kuliko yaliyowahi kutolewa kwa wanadamu linapatikana ktk ujumbe wa malaika wa tatu (Ufunuo 14:9-12). Ni lazima iwe ni dhambi ya kutisha ambayo inasababisha kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu isiyochanganywa na rehema. Watu hawapaswi kuachwa gizani kuhusu jambo hili muhimu.
Onyo dhidi ya dhambi hili halina budi kutolewa kwa ulimwengu kabla ya kuja kwa hukumu za Mungu, ili wote wajue ni kwa nini hukumu hizi ni lazima zitolewe na waweze kuwa na fursa ya kuziepuka.
Katika suala la pambano kuu, makundi mawili yaliyo dhahiri, na yanayotofautiana yanajitokeza.
Katika kundi moja kuna kila mtu ambaye atamsujudu "huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa ktk kipaji cha uso wake, au ktk mkono wake" na hivyo wanajiletea juu yao hukumu za kutisha zilizotangazwa na malaika wa tatu. Kundi lingine, likiwa kinyume kabisa na dunia, ni la wale "wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu." Ufunuo 14:9,12.

EmoticonEmoticon