Wakati ule ambapo makanisa makubwa ya Marekani, yakiungana ktk vipengele vile vya mafundisho ya imani yanayifanana miongoni mwao, yatakaposhawishi nchi hii ili kushurutisha sheria zao na kuendeleza taasisi zao, hapo ndipo Marekani ya Kiprotestanti itakuwa imefanya sanamu ya mamlaka ya Kirumi, na adhabu kwa raia wasioafikiana na sheria hizo itatolewa bila kuepukika...
Ulazimishaji wa utunzaji wa Jumapili kwa upande wa makanisa ya Kiprotestanti ni ulazimishaji wa kuabudu upapa.....
Katika kitendo hasa cha kulazimisha wajibu wa kidini kwa kutumia mamlaka za kidunia, makanisa haya yatafanya sanamu ya mnyama; hivyo ulazimishaji wa utunzaji wa siku ya Jumapili ktk nchi ya Marekani utakuwa ni ulazimishaji wa ibada ya mnyama na sanamu yake. - GC 445, 448, 449 (1911).
Wakati Uprotestanti utakaponyoosha mkono wake kulivuka lile shimo kubwa na kuukumbatia mkono wa mamlaka za Kirumi, wakati utakaponyoosha mkono wake kuelekea kuzimuni ili kukumbatiana mikono na umizimu, wakati, wakiwa chini ya ushawishi wa muungano huu wa washiriki watatu, nchi yetu itaikana kila kanuni ktk Katiba yake kama serikali ya Kiprotestanti na ya Kijamhuri na itaweka mazingira kwa ajili ya uenezaji wa udanganyifu na ulaghai wa kipapa, hapo ndipo tutakapojua kuwa wakati umekuja kwa ajili ya utendaji wa ajabu wa Shetani na kuwa mwisho uko karibu. - 5T 451 (1885).

EmoticonEmoticon