UHALIFU, NJAA, TAUNI.



Shetani anatenda kazi ktk hewa; anatia sumu hewa, nasi hapa tunamtegemea Mungu kwa ajili ya maisha yetu-maisha yetu ya sasa na ya milele. Nasi tukiwa ktk nafasi tuliyomo sasa, tunahitaji kuamka kabisa, tukijitoa kikamilifu, kuongoka kabisa, na kujikabidhi kikamilifu kwa Mungu. Lakini tunaonekana kukaa kana kwamba tumepooza. Mungu wa mbinguni, utuamshe! -2SM 52 (1890).

Mungu hakuzuia nguvu za giza kuendeleza kazi yake ya kuchafua hewa, ambayo ni mojawapo ya vianzo vya uhai na lishe, kwa hewa nzito ya kufisha. Sio tu kwamba maisha ya mboga yanaathirika bali binadamu huteseka kutokana na tauni. . . . Vitu hivi ni matokeo ya matone yatokayo ktk vichupa vya gadhabu ya Mungu yanayonyunyizwa duniani, nayo ni mawakilisho tu hafifu ya kile kitakachokuwako muda mfupi ujao. -3SM 391 (1891).

Njaa zitaongezeka. Magonjwa ya mlipuko yatafagilia mbali maelfu. Hatari zinatuzunguka pote kutoka ktk nguvu nje na utendaji wa kishetani kutoka udhibiti wa ndani, lakini nguvu za Mungu sasa zinatenda kazi.-19 MR 382 (1897).

Nimeonyeshwa kuwa Roho wa Bwana anaondolewa duniani.
Nguvu za Mungu zinazotuhifadhi muda si mrefu zitazuiwa kwa wale wote wanaoendelea kutojali amri zake. Taarifa za biashara za utapeli, mauaji, uhalifu, wa kila namna zinatujia kila siku. Uovu unaendelea kuwa jambo la kawaida kiasi kwamba haushtui tena hisia za watu kama ilivyokuwa hapo kwanza. - Letter 258, 1907

Image may contain: 1 person
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.