Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. Nehemia 2:6.
Wakati Nehemia akiomba msaada wa Mungu, hakukunja mikono yake, kwa kujisikia kwamba hakuwa na kazi au wajibu mwingine zaidi katika kukamilisha kusudi lake la kuirejesha Yerusalemu. Huku akitumia tahadhari kwa namna inayovutia na busara aliendelea kufanya mipango yote iliyokuwa muhimu katika kuhakikisha mafanikio ya shughuli….
Kielelezo cha mtu huyu mtakatifu yapasa kiwe fundisho kwa watu wa Mungu wote, kuwa si kwamba waombe kwa imani tu, lakini wafanye kazi kwa bidii na kwa uaminifu. Ni matatizo mangapi tunayokabiliana nayo, ni mara ngapi tunazuia utendaji wa Mpaji kwa niaba yetu, kwa sababu tahadhari, busara na uangalifu wa hali ya juu vinaonekana kama havihusiki sana na dini! Hili ni kosa kubwa sana. Ni wajibu wetu kuendeleza na kufanyia mazoezi kila uwezo ambao utatufanya tuwe na wafanyakazi wa Mungu walio na ufanisi zaidi. Kufikiri kwa uangalifu na mipango yenye ukomavu ni muhimu katika kufanikisha shughuli takatifu leo kama ilivyokuwa wakati wa Nehemia… Watu wa maombi yapasa wawe watu wa vitendo. Wale walio tayari na wenye nia, watapata njia na namna ya kufanya kazi. Nehemia hakutegemea mambo yasiyo na uhakika. Nyenzo alizopungukiwa alizitafuta kutoka kwa wale waliokuwa tayari kuzitoa.
Bado Mungu anagusa mioyo ya wafalme na watawala kwa niaba ya watu wake. Wale wanaofanya kazi kwa ajili ya Mungu yapasa watumie nafasi ya msaada ambao yeye huwasukuma watu wautoe kwa ajili ya kuendeleza kazi yake. .. Watu hawa wanaweza wasiipende kazi ya Mungu, wanaweza wasiwe na imani katika Kristo, wanaweza wasijue neno lake; lakini matoleo yao katika eneo hili yasikataliwe….
Kadiri tunavyoendelea kuwa katika dunia hii, kadiri Roho wa Mungu anavyoendelea kupambana na wanadamu, vivyo hivyo inatupasa kupokea fadhila na kuzitoa. Inatupasa kuipa dunia nuru ya ukweli, kama inavyodhihirishwa kwenye Maandiko; nasi inatupasa kupokea kutoka duniani kile ambacho Mungu anawagusa watu watoe kwa ajili ya kazi yake… Laiti Wakristo wangetambua zaidi na zaidi kikamilifu kwamba wamepewa fursa ya pekee na ni wajibu wao, huku wakiendeleza kanuni zilizo sahihi, kutumia kila fursa iliyotumwa na Mbingu kwa ajili ya kuendeleza ufalme wa Mungu hapa duniani!
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon