KUSUDI TAKATIFU



Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako,…unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu.
Nehemia 1:11.

Nehemia, mmoja kati ya Waebrania waliokuwa uhamishoni, alikuwa na nafasi yenye mvuto na heshima kwenye ikulu ya Uajemi. Akiwa mnyweshaji wa mfalme alikuwa na uhuru kwenye makao ya kifalme… Kupitia kwa mtu huyu…Mungu alikusudia kuleta baraka kwa watu wake kwenye nchi ya baba zao…. Huyu mzalendo wa Kiebrania alijua kwamba siku za jaribio zilikuwa zimeifikia Yerusalemu, mji uliochaguliwa. Waliorudishwa kutoka uhamishoni walikuwa wakipata shida kutokana na mateso na fedheha… Kazi ya urejeshwaji ilizuiwa, huduma za hekalu zikavurugwa na watu wakawa macho wakati wote kutokana na ukweli kwamba kuta za mji zilikuwa bado katika hali ya uharibifu kwa kiasi kikubwa…

Mara kwa mara Nehemia alikuwa amemimina moyo wake kwa niaba ya watu wake. Lakini sasa alipokuwa akiomba kusudi takatifu lilijengwa akilini mwake. Alikusudia kwamba kama angepata kibali cha mfalme na msaada wa muhimu katika kupata vifaa na nyenzo, yeye mwenyewe angechukua jukumu la kujenga upya kuta za Yerusalemu…

Nehemia alingoja kwa miezi minne ili kupata fursa ifaayo kwa ajili ya kuwasilisha ombi kwa mfalme… Alikuwa na wajibu mtakatifu ambao ilimpasa kuutimiza, ambao kwa huo alihitaji msaada wa mfalme; naye akatambua kuwa ilitegemea sana namna alivyokuwa awasilishe suala hilo kwa namna ambayo angepata ukubali na kutoa msaada wake. Anasema, “Nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni.” Katika lile ombi fupi, Nehemia aliingia katika kuwepo kwake Mfalme wa wafalme na akafanikiwa kupata uwezo ambao ungeweza kubadili mioyo kama mito ya maji inavyobadilishwa.

Kuomba kama Nehemia alivyoomba wakati wa hitaji lake ni muhimu na ni kitu Mkristo anachoweza kufanya akiwa katika mazingira ambapo njia zingine zote za maombi zinaonekana kutokuwezekana… Nyakati za matatizo ya ghafla au hatari moyo unaweza kupeleka kilio chake cha hitaji la msaada kwake Yeye ambaye ameahidi kuwa msaada kwa waaminifu wake, wanaoamini wakati wowote wanapomuita. Katika kila mazingira, kwenye kila hali, nafsi iliyolemewa kwa huzuni na wasiwasi, au wanaposhambuliwa vikali na majaribu, wanaweza kupata uhakika, kuungwa mkono na kupata msaada kutoka kwa upendo usioshindwa na nguvu ya Mungu anayetunza agano.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23)

No automatic alt text available.
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.