IMANI JUU YA KUONGEA NA MIZIMU.......Sehemu ya 5



Inaendelea.......
Nabii Isaya asema hivi: "Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?! Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi" Isaya 8:19,20.
Kama wanadamu wangekubali kuupokea ukweli unaoelezwa dhahiri ktk Biblia, ya kwamba wafu hawajui kitu, ndipo wangeweza kuyaona maneno na maonyesho ya pepo kwamba ni kutenda kwake Shetani kwa uwezo na ishara na ajabu za uongo.
Lakini kwa kuwa ni vigumu kwao kuacha kufuata mapenzi yao ya nia ya mwili, wasitake kujitenga na dhambi ambazo wanapenda kuzifanya, wingi wa watu wameyafumba macho yao wasione nuru; tena wanaendelea mbele bila kujali maonyo, wakati Shetani anapoweka tanzi lake la kuwategea, hao nao hushikwa naye.
"Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa," kwa hiyo "Mungu awaletea nguvu ya upotevu wauamini uongo." 2 Wathesalonike 2:10,11.

Wale wanaoyakataa mafundisho juu ya kuongea na mizimu (Spiritualism), si kwamba wanashindana na wanadamu tu, bali wanashindana na Shetani mwenyewe na malaika zake. Wameingia ktk vita juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza la ulimwengu huu, na juu ya majeshi ya pepo wabaya ktk ulimwengu wa roho. Shetani hataacha nafasi hata kidogo asipofukuzwa na uwezo wa wajumbe watokao mbinguni.
Inawapasa watu wa Mungu kuwa tayari kumkabili kama Mwokozi wetu alivyomkabili na maneno haya, "Imeandikwa." Hata sasa Shetani anaweza kuyataja mafungu ya Biblia kama alivyofanya ktk siku za Kristo, naye atayageuza vibaya mafundisho ya Biblia ili yapate kulingana na madanganyifu yake.
Lakini maneno yaliyoandikwa dhahiri ktk Biblia yanakuwa silaha za kutosha kushinda ktk kila shindano...

Itaendelea.......

Image may contain: one or more people and crowd
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.