Inaendelea...
Uchawi wa Namna ya Kisasa
Jina hasa la uchawi linadharauliwa siku hizi. Habari inayosema ya kwamba wanadamu wanaweza kuongea na pepo wachafu inafikiriwa kuwa hadithi ya Zama za Giza. Lakini imani hii juu ya kuongea na mizimu (yaani Spiritualism), inayofuatwa na watu maelfu, naam, watu milioni nyingi, na ambao imepata nafasi ya kupenya ktk mambo ya elimu, na ambayo imeingia ktk makanisa, tena inapendelewa sana na watu wa baraza kuu na ktk majumba ya wafalme-udanganyifu mkubwa huu wa siku hizi sio jambo la kigeni hasa, lakini ni kuamsha kwa namna nyingine uchawi ule ule uliolaumiwa na kukatazwa ktk siku za kale.
Shetani huwadanganya watu siku hizi kama vile alivyomdanganya Hawa ktk bustani ya Edeni, kwa kuichochea tamaa ya kupata ujuzi isiyo halali yake. Shetani asema "Mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya." Mwanzo 3:5. Lakini ujuzi unaoletwa na ile dini ya kuamini pepo ndiyo ile iliyosimuliwa na mtume Yakobo: "Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na Shetani."
Yakobo 3:15.
Mkuu wa giza yu mwenye akili nyingi, naye huleta majaribu ya hila akigeuza majaribu na kuyafanyiza kufaa kwa kuwashika watu wa kila namna, wenye daraja na hali na uwezo mbali mbali. Hutumia "madanganyo yote ya udhalimu" ili kuwatawala wanadamu, lakini hawezi kuyatimiza mapenzi yake kwao ila tu kama wakikubali kushindwa na majaribu yake. Wale wanaojitia chini ya utawala wake kwa kuyaendeleza matendo yao mabaya na kukuza tabia zao zilizo mbaya, hawawezi kuufahamu mwisho wa mwenendo wao. Yule mwovu huwajaribu kabisa, ndipo huanza kuwatumia kwa kuwaharibu watu wengine pia.
Itaendelea.......

EmoticonEmoticon