IMANI JUU YA KUONGEA NA MIZIMU..... Sehemu ya 1



Imani ya kwamba mwanadamu ana roho isiyoweza kufa imefanya njia tayari kwa dini ya siku hizi ya kuongea na mizimu. Ikiwa ni kweli ya kuwa wafu hukubaliwa kwenda mbele za Mungu na malaika watakatifu, na kupewa maarifa yanayozidi yale waliokuwa nayo zamani, je, wasingeweza kurudi duniani kuwafundisha walio hai?
Wale wanaoamini ya kwamba wanadamu wanaendelea kuishi peponi baada ya kufa, wanawezaje kukataa mafundisho ya uongo yanayokuja kwao kama ni nuru ya Mungu inayoletwa na pepo zilizotukuzwa?
Hapa kuna njia ambayo watu hudhani ya kwamba ni takatifu lakini hutumiwa na Shetani ili ayatimize makusudi yake. Malaika waovu wanaofanya mapenzi ya Shetani anapojidai ya kwamba anawawezesha walio hai kuzungumza na wafu, ndipo anapotumia uwezo wake wa giza kwa kuwadanganya ktk fikara zao.

Shetani ana uwezo hata kufanya watu watokewe na mifano ya rafiki zao waliokwisha fariki. Mfano huu ni kamili; maneno na sauti huigizwa sawa sawa. Wengi hufarijiwa kwa kuamini ya kwamba wapenzi wao wamo ktk hali ya heri mbinguni, na bila kutambua ya kwamba wamo hatarini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.

Itaendelea.......

 Image may contain: 3 people, people standing
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.