BABA MWOGA



“Nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.” 1 Samweli 3:14.

Eli hakutawala vyema nyumba yake kulingana na maelekezo ya Mungu kuhusu serikali ya familia. Eli alifuata matashi yake. Wengi wanafanya makosa ya jinsi iyo hiyo leo. Wanafikiri wanajua mbinu bora ya kuelimisha watoto wao kuliko njia ile Mungu aliyoielekeza kwenye Neno lake. Wanawapa mielekeo potofu kwa kisingizio kuwa-- “Ni wadogo mno wasiostahili adhabu. Subiri hadi wawe wakubwa, uweze kujadili pamoja nao.” Hivyo tabia mbaya inaachwa ikue hadi inakuwa sehemu ya maisha yao. Watoto wanakua pasipo nidhamu, wanakua na sifa za kitabia zilizo laana kwao wenyewe na zenye uwezekano wa kuambukiza sumu ya uovu kwa wengine.

Kwa upambanishi na kisa cha uaminifu cha Ibrahimu, na maneno ya sifa njema yaliyoongelewa kwake; kipo kisa cha Eli, ambaye aliwabakiza watoto wake katika ofisi ya ukuhani wakati wanatenda uovu mkuu. Hapa lipo somo kwa wazazi wote. . . Uovu, pasipo ukemeaji wo wote, uliruhusiwa na Eli. Matokeo yake ni dhambi ambayo haiwezi kupatanishwa kwa kafara au dhabihu milele zote.

Wakati wengine hutenda kosa kwa ukali kupita kiasi, Eli alikuwa kinyume. Alikuwa mpole kupindukia. Makosa ya wanawe yalipuuziwa utotoni mwao, na kutokemewa wakati wa ujana wao. Maagizo ya wazazi yalipuuziwa, na baba hakuweza kusimamia utii.

Watoto waliona kuwa wanaweza kushikilia usukani wa utawala, na kila siku waliendeleza fursa hiyo. Kadri wanawe walivyoongezeka umri, walikoma kabisa kumheshimu baba yao mwoga. Waliendeleza maisha yao ya dhambi pasipo kuzuiwa. Alijadiliana nao na kuwashauri, ila neno lake halikutiiwa. Dhambi za kutisha na uhalifu uliokithiri ulitendwa kila siku na vijana hao, hadi BWANA mwenyewe akatoa hukumu kwa hawa wahalifu wa sheria yake.

Bwana mwenyewe alitangaza kuwa kwa dhambi ya wana wa Eli hakuna kafara au dhabihu ya kuleta upatanishi kwa ajili yao. Anguko lao ni kuu, na la kutisha jinsi gani—watu ambao walikabidhiwa majukumu matakatifu, kukataliwa na kuangamizwa pasipo huruma, na Mungu mwenye haki na mtakatifu!

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.