Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke ktk wafu,
Na Kristo atakuangazia.
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Waefeso 5:14-17.
"Wakati tabia ya Kristo itakapoakisiwa kwa ukamilifu ndani ya watu wake, hapo ndipo atakapokuja kuwataka kwa halali kuwa wao ni watu wake mwenyewe. Ni haki ya kila Mkristo, sio tu kutazamia, bali kuharakisha kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo" (COL 69).

EmoticonEmoticon