Nawe, Bwana, usinizuilie rehema zako, fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.
Zaburi 40:11.
🏾Dini ya Kristo itainua maisha hadi kufikia kiwango cha juu. Kazi inayofanyika ndani ya Roho wa Mungu hunyenyekeza kiburi cha mwanadamu, kwa kutusababisha kuelewa kitu kuhusu rehema za pekee na wema utokanao na upendo wa Mungu… Unapogundua upungufu wako mwenyewe na kutazama chanzo cha nguvu zako, kisha usihi kwa shauku ukisema, “Ee Bwana, usinizuilie rehema zako, fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima,” utapata nuru…
🏾Huwezi kuwa na imani kwamba Bwana atakuhifadhi kwa wema wake na kudumu kukutunza kwa kweli yake, kama hujiweki mwenyewe kwenye mkondo wa nuru. Kwa sababu hiyo, epuka marafiki wabaya na uchague marafiki wazuri. Mbegu ya ukweli inayopandwa moyoni lazima ipokee nuru inayong’aa ya Jua la haki ili ipate kukua. Mbegu za ile kweli ambazo hazichipui na kukua, mara hupoteza nguvu yake ya kuchipua na hivyo huangamia. Lakini magugu ya tabia mbaya yatachipua na kuchanua. Mimea ya thamani ya upendo, furaha, subira, staha, upole na unyenyekevu inahitajika kukuzwa kwa uangalifu kama kweli inategemewa ikue na kuwa bora.
🏾Usiridhishwe na utauwa wa juu juu, lakini rafiki yangu kijana, kua katika neema na ufahamu wa Yesu Kristo. Je, unayo maendeleo yoyote? Mmea wa neema unakuwa na kuwa mti, au unanyauka? Jiweke mwenyewe kwa unyenyekevu na tena mara kwa mara kwenye kiti cha neema na umwambie Yesu kila hitaji ulilo nalo na usidhani kwamba kwake kuna kitu chochote kilicho kidogo hata asikitambue. Bwana anapenda umtafute tena umwambie juu ya majaribu yako, kama mtoto awezavyo kuongea na mzazi wake. Unapoomba, amini Yesu anakusikia na atatenda mambo unayomuomba. Onesha kwamba unamtegemea Yesu kikamilifu na daima ujitahidi kutenda yale unayojua kwamba yanampendeza nawe utakuwa na amani katika Kristo.

EmoticonEmoticon