baada ya kuondolewa kigundua makosa, Shetani alitenda kama apendavyo. Unabii ulitangaza kuwa upapa ungekusudia "kubadili majira na sheria" Daniel 7:25. Kazi hii hakuchelewa kuijaribu. Ili kuwapa waongofu kutoka ktk upagani kitu mbadala cha kuabudu sanamu, na hivyo kukuza ukubali wao wa Ukristo kijina tu, Ibada ya kuabudu sanamu na Kumbukumbu za watakatifu wa zamani ziliingizwa polepole ktk Ibada ya Kikristo.
Amri ya baraza kuu hatimaye ilithibitisha mfumo huu wa ibada ya sanamu. Ktk kukamilisha kazi hii ovu, Rumi ilithubutu kufuta kutoka ktk sheria ya Mungu amri ya pili, ambayo inakataza Ibada ya sanamu, na kuigawanya amri ya kumi, ili kudumisha idadi.
Roho ya maridhiano na upagani ilifungua njia kwa ajili ya kuidharau zaidi mamlaka ya Mbingu. Shetani aliigeuza amri ya nne pia, na kukusudia kuiweka kando Sabato ya awali, siku ambayo Mungu aliibariki na kuitakasa, na badala yake kuitukuza siku kuu iliyoshehelekewa na wapagani kama "siku ya kuheshimiwa ya jua." Badiliko hili mwanzoni halikujaribiwa waziwazi. Ktk Karne za awali Wakristo wote waliitunza Sabato ya kweli.
Walikuwa na Wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu, na, huku wakiamini kuwa sheria yake haibadiliki, kwa bidii walitunza utakatifu wa maagizo yake. Lakini Shetani alitenda kwa werevu mno kupitia kwa wakala wake ili kutimiza kusudi lake. Ili kuekekeza macho na fikra za watu juu ya Jumapili, ilifanywa kuwa sikukuu kwa ajili ya heshima ya ufufuko wa Kristo. Huduma za kidini zilifanyika ktk siku hii, lakini tena ilichukuliwa kuwa siku ya mapumziko, na Sabato ilitunzwa kwa utakatifu.
Wakati ambapo alikuwa bado mpagani, Konstantino alitoa amri iliyoelekeza utunzaji wa Jumapili kama sikukuu ya taifa ktk Himaya yote ya Kirumi. Baada ya uongofu wake alibaki kuwa mtetezi mkuu wa Jumapili, na ndipo aliposhurutisha utiifu wa amri yake ya kipagani kwa ajili ya maslahi ya imani yake mpya. Lakini heshima ilipewa siku hii bado haikutosheleza kwa wakati ule kuwazuia Wakristo kuiheshimu Sabato ya kweli kuwa takatifu kama alivyo Bwana. Hatua nyingine lazima ichukuliwe: sabato ya uongo lazima iinuliwe kuwa sawa na ile ya kweli. Miaka michache baada ya Konstantino kutoa amri yake, Askofu wa Rumi aliipa jina Jumapili na kuiita siku ya Bwana. Kwa njia hii pole pole watu walianza kuiona kuwa ilikuwa na kiwango fulani cha utakatifu. Lakini bado Sabato ya mwanzo ilitunzwa.
Mdanganyifu mkuu alikuwa bado hajakamilisha kazi yake. Alidhamiria kuuweka ulimwengu wa Kikristo chini ya bendera yake na kutumia uwezo wake kupitia kwa naibu wake, Papa mwenye kujisifu aliyedai kuwa ni mwakikishi wa Kristo. Kupitia kwa wapagani walioongoka nusunusu, maaskofu wenye tamaa ya makuu, na washiriki wa kanisa wenye kuipenda dunia alikamilisha kusudi lake. Mara kwa mara mabaraza makuu yalifanyika, ambapo watu wenye vyeo kanisani walikusanyika kutoka duniani kote. Karibu ktk kila baraza Sabato ambayo Mungu aliianzisha ilikandamizwa chini kidogo wakati Jumapili ilitukuzwa kwa kiwango hicho hicho. Hivi ndivyo ambavyo sikukuu ya kipagani hatimaye ilikuja kuheshimiwa kama taasisi ya Mungu na huku Sabato ya Biblia ilitangazwa kuwa kumbusho la dini ya Kiyahudi, na watunzaji wake wakatangazwa kuwa wamelaaniwa.

EmoticonEmoticon