NI KRISTO PEKEE




Mtu ambaye atamwungamia Kristo, lazima Kristo awe anaishi ndani yake. Mitume wake lazima wawe wakinena kwa ufasaha mafundisho yake.

Lakini walisipokuwa nayo tabia ya Kikristo halisi, tabia ya unyenyekevu na upendo, hawawezi kumwungamia. 

Roho ambayo ni kinyume cha Roho yake humkana.

Watu umkana Kristo kwa kusema misemo mibaya, kwa maongezi ya kijinga, kwa maneno ya ovyo ambayo siyo ya kweli, au kwa maneno yasiyo mema.

Wanaweza kumkana kwa kutosaidia mzigo wa maisha ya watu, na kwa kujiunganisha na kawaida za dunia, na kwa hali isiyokuwa ya utu mwema, na kwa njia ya kukuza hali ya ubinafsi, na kwa kuwa na mashaka, na kuwa na uchokozi.

"Mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni "
"EGWhite Tumaini la Vizazi Vyote uk 196"

Maneno yanayokaribiana na onyo la Kristo kuhusu kumtukana Roho Mtakatifu, ni yale ya usemi mbaya.

Maneno ndiyo yanayoonyesha tabia ya mtu alivyo.

"Kinywa cha mtu huyanena yale yaujazayo moyo wake."

Maneno yana uwezo wa kuonyesha tabia ya mtu. Mtu hupimwa kwa maneno anenayo.
Mara nyingi maneno ya ubishi huongozwa na Shetani, husemwa tu bila kufikiriwa, lakini matokeo huonyesha mambo ya moyoni.
Maneno yasemwayo ktk utani hupitia hivyo bila kusahihishwa.
Husemwa tu kwa namna hiyo.
"E. G. White, "Tumaini la Vizazi Vyote, uk 176"

Image may contain: 1 person, text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.