Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.
Zaburi - 27:4.
Uwezo uliotukuka unafikika kwa kila mmoja. Chini ya usimamizi wa Mungu, mwanadamu anaweza kuwa na moyo usiopotoka, uliotakaswa, ulioadilishwa, mwungwana. Kupitia katika neema ya Kristo, moyo wa mwanadamu unafanywa ufae kumpenda na kumtukuza Mungu, Mwumbaji.
Bwana Yesu alikuja kwenye dunia yetu kumwakilisha Baba… Kristo alikuwa mfano halisi wa nafsi ya Baba; naye alikuja kwenye dunia yetu kumrejeshea mwanadamu sura ya kimaadili ya Mungu, ili kwamba hata ingawa mwanadamu ameanguka, apate kutiwa muhuri wa sura na tabia ya Mungu kwa njia ya kutii amri za Mungu.
Mungu anataka watoto wake wapendeze, siyo kwa mapambo bandia, bali kwa uzuri wa tabia, uzuri wa wema na upendo, ambao utafanya mioyo yao ifungwe kwa furaha na raha.
Yapasa WASICHANA wafundishwe kwamba _HAIBA_ ya kweli ya kike haipo katika uzuri wa umbo au uso, wala katika kuwa na mafanikio fulani; bali katika upole na roho ya utulivu, katika subira, ukarimu, wema na utayari wa kutenda na kuteseka kwa ajili ya wengine. Inapasa wafundishwe kufanya kazi, kusoma kwa ajili ya kusudi maalum, kuishi kwa malengo, kumtumainia na kumcha Mungu na kuheshimu wazazi wao. Kisha umri wao unapoendelea, watakuwa na mioyo safi zaidi, watazoea kujitegemea na kupendwa. Itakuwa haiwezekani kumdhalilisha mwanamke kama huyu. Ataepuka majaribu na mitihani ambayo imeangamiza wengi.
Kristo alitumwa kama kielelezo chetu. Je, hatutaonesha kwamba tunao upendo wake na wema wake wote na…. haiba yake? Upendo wa Yesu Kristo utatawala tabia na maisha yetu na maongezi yetu yatakuwa matakatifu na tutakuwa tumejikita kwenye mambo ya kimbingu.

EmoticonEmoticon