
"Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Yohana 14:18."
Kristo alitamani kwamba wanafunzi wake wapate kufahamu kuwa asingeliwaacha yatima. “Sitawaacha ninyi yatima” Alitamka; “naja kwenu. Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.” (Yohana 14:18, 19) Uhakikisho tukufu wenye thamani kuu wa uzima wa milele! Ijapokuwa ilibidi asiwepo, uhusiano wao pamoja naye ulitakiwa kuwa ule wa mtoto kwa mzazi wake.
“Siku ile” Alisema, “ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.” (Yohana 14:20). Alijitahidi kushawishi akili za wanafunzi kwa tofauti iliyopo baina ya wale walio wa ulimwengu na wale walio wa Kristo. Alikuwa anakaribia kufa, lakini alitamani wapate kutambua kuwa angeliishi tena. Na ijapokuwa, baada ya kupaa kwake, asingelikuwapo kwao, lakini bado kwa imani wangeliweza kumwona na kumfahamu, na angelikuwa na shauku ile ile ya upendo kwao kama wakati alipokuwa pamoja nao. …
Maneno yaliyozungumzwa kwa wanafunzi yanakuja kwetu kupitia kwa maneno yao. Mfariji ni wetu pia kama alivyo wao, katika nyakati zote na kila mahali, katika huzuni zote na katika mateso yote, wakati mwonekano unaelekea kuwa giza na siku za usoni kutatiza, na tunahisi kutokuwa na msaada na wapweke. Hizi ni nyakati ambapo Mfariji atatumwa kuwa jibu la maombi ya imani.
Hakuna mfariji aliye kama Kristo, aliye mpole, mkweli. Anaguswa na hisia za udhaifu wetu. Roho wake anazungumza na moyo. Hali zinaweza kututenganisha kutoka kwa rafiki zetu; bahari pana, yenye mawimbi inaweza kuvuma kati yetu na wao. Ingawa urafiki wao wa dhati unaweza kuwapo bado, inawezekana wasiweze kuudhihirisha kwa kututendea kile ambacho kingelipokelewa kwa shukurani. Lakini hakuna hali, hakuna umbali, unaoweza kututenga kutoka kwa Mfariji wa kimbingu. Po pote tulipo, po pote tunapoweza kwenda, siku zote yuko pale, yule aliyetolewa kuchukua nafasi ya Kristo, ili kutenda badala yake. Siku zote yuko mkono wetu wa kuume, ili kuzungumza maneno ya upole yenye kutuliza, kusaidia, kuhimili, kutetea, na kuchangamsha.
Uwezo wa Roho Mtakatifu ndio maisha ya Kristo rohoni. Roho huyu hutenda kazi ndani ya na kupitia kwa kila mtu anayempokea Kristo. Wale wanaotambua ukaaji moyoni wa Roho huyu hudhihirisha matunda yake-upendo, furaha, amani, uvumilivu, upole, wema, imani. - Review and Herald, Oct. 26, 1897.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon