KUJENGA JUU YA MWAMBA

Image may contain: text, outdoor and water






Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
Mathayo 7:24.

Hapo uliposimama leo ukiona dosari za tabia yako unapoilinganisha na kiwango cha Mungu cha kimaadili, hutasema, “Nitakomboa yaliyopita; nitaenda kufanya kazi kwenye shamba la mizabibu la Bwana”? Kwa imani iliyo hai, je hutashikilia ahadi za Mungu na kuchukua haki ya Kristo na kuona nuru ya mbinguni iking’aa maishani mwako? Inakupasa umlete Kristo kwenye kila wazo lako na tendo lako. Kiungo chenye kasoro kwenye mnyororo huufanya ukose thamani na dosari kwenye tabia yako itakufanya usifae kuingia kwenye ufalme wa mbinguni.

Ni lazima uweke kila kitu vizuri. Lakini huwezi kufanya kazi hii kuu bila msaada wa kimbingu. Je, uko tayari kukubali ahadi za Mungu na kuzifanya ziwe zako kabisa kwa imani iliyo hai katika neno lake lisilobadilika? Inakupasa utembee kwa imani, sio kwa hisia. Hatuhitaji dini ya misisimko; lakini tunataka dini ambayo msingi wake ni imani yenye akili. Imani hii inakuwa imesimama kwenye mwamba wa milele wa Neno la Mungu. Wale wanaotembea kwa imani, wakati wote huwa wanatafuta ukamilifu wa tabia kwa kudumu katika kumtii Kristo.

Nahodha wa wokovu wetu ametupatia maagizo na inatupasa tuoneshe utii usioyumba; lakini kama tukifunga Kitabu kinachodhihirisha mapenzi yake, na wala hatuulizi, hatutafuti, au kutaka kuelewa, tunawezaje kutimiza wajibu wake? Hatimaye tutakutwa tukiwa tumepungua, kama tukienda katika mwelekeo huu…

Tunaijia zahama, nami ninaogopeshwa na roho zetu. Kwa nini tunaona wanaume wakiiacha imani? Je, tupo kwenye nafasi ambapo tutajua tunachokiamini na tusitupwe nje? Kwa watu kuacha ukweli, hilo lisituvunje mioyo hata kidogo, bali litusaidie kutafuta kwa bidii zaidi baraka ya Mungu. Siyo elimu, au talanta, au nafasi za watu, zitakazowaokoa. Inatupasa tutunzwe kwa nguvu ya Mungu kwa njia ya imani hadi tuufikie wokovu.

Unasimamaje mbele za Mungu leo? Swali sio kwamba utasimamaje siku ya taabu, au wakati fulani ujao? Lakini roho yako ikoje leo? Utaenda kazini leo? Tunataka uzoefu wa mtu binafsi, mmoja mmoja leo. Leo, tunamhitaji Kristo akae pamoja nasi. – Review and Herald, April 9, 1889.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.