
Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
2 Timotheo 4:3, 4.
Mengi yamesemwa kuhusu kupewa Roho Mtakatifu na kwa baadhi ya watu hili linafasiriwa kuwa ni jeraha kwa makanisa. Uzima wa milele ni kupokea vile vilivyo hai ambavyo vimo kwenye Maandiko na kutenda mapenzi ya Mungu. Huku ndiko kula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu. Kwa wale wafanyao hivi, uzima na kuishi milele vinawekwa wazi kupitia katika injili , kwani Neno la Mungu ni hakika na kweli, roho na uzima. Ni faida kwa wote wanaomwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wao binafsi kujilisha Neno la Mungu. Mvuto wa Roho unatafsiri Neno hilo, Biblia, ukweli wa milele, ambao kwa mtafiti mwenye maombi linampa nguvu na uthabiti kiroho.
Kristo alisema, “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia” (Yohana 5:39). Wale wanaochimba chini zaidi ya uso wa nchi huwa wanagundua vito vya ukweli vilivyofichwa.
Roho Mtakatifu yuko pamoja na mtafutaji wa dhati. Nuru yake hung’aa kwenye Neno, ikiutia kama muhuri ukweli moyoni kwa umuhimu mpya. Mtafiti anajazwa kwa hali ya kujisikia amani na furaha ambayo kamwe anakuwa hajawahi kuisikia kabla. Thamani ya ile kweli inaonekana kwa namna ambayo haijapata kuwa hivyo kabla. Nuru mpya ya kimbingu inang’aa kwenye neno, ikiliangaza kana kwamba kila herufi imetiwa rangi ya dhahabu. Mungu mwenyewe anakuwa amenena na akili na moyo, akilifanya Neno roho na uzima.
Kila mtafutaji wa kweli wa Neno huinua moyo wake kwa Mungu, akiomba msaada wa Roho. Naye mara anagundua kile kinachomchukua juu ya kauli zote za kubuni za yule ambaye anayejiita kuwa mwalimu, ambaye nadharia zake zilizo dhaifu, zinazoyumbayumba haziungwi mkono na Neno la Mungu aliye hai.
Nadharia hizi ziligunduliwa na watu ambao walikuwa hawajajifunza fundisho la kwanza kuu, kwamba Roho wa Mungu na uzima vyote vimo ndani ya Neno lake. Kama wangekuwa wamepokea mioyoni ukweli huu wa milele uliomo kwenye Neno la Mungu, wangeona jinsi jitihada zote za kupata kitu fulani kipya ili kutengeneza hisia zilivyo nyonge na zisivyo na maana. Wanahitajika kujifunza kanuni za awali kabisa za Neno la Mungu.
Selected Messages, vol. 2, uk. 38,39.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon