
"Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi".
Ebra 4:15.
Kristo anaishi ndani yake yeye anayempokea kwa imani. Ingawa majaribio yanaweza kuja rohoni, lakini bado uso wa Bwana utakuwa pamoja nasi. Kichaka kinachowaka moto ambacho ndani yake mlikuwamo na uwapo wa Bwana hakikuteketea. Moto haukufisha unyuzi hata mmoja wa matawi. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa wakala dhaifu wa kibinadamu ambaye anaweka tumaini lake kwa Kristo. Moto wa tanuri la majaribu unaweza kuwaka, mateso na majaribio yanaweza kuja, lakini ni takataka peke yake ndio itakayotekekezwa. Dhahabu itang’aa zaidi kwa sababu ya mchakato wa utakaso.
Ni mkuu zaidi yeye aliye katika moyo wa waaminifu kuliko yule aliye katika mioyo wa wasioamini. Usilalamike kwa uchungu kuhusu majaribio yanayokuja juu yako, bali elekeza macho yako kwa Kristo, ambaye amevika uungu wake kwa ubinadamu, ili kwamba tupate kuelewa jinsi ilivyo kuu shauku yake kwetu kwa kuwa amejitambulisha na mateso ya wanadamu. Alionja kikombe cha huzuni ya mwanadamu, aliteswa katika mateso yetu yote, alifanywa kuwa mkamilifu kupitia kwa mateso, katika kila hali alijaribiwa kama mwanadamu anavyojaribiwa, ili kwamba aweze kuwaokoa wale walio katika majaribu.
Anasema, “nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri” (Isaya 13:12). Atamfanya mwanadamu kuwa wa thamani kubwa kwa kukaa pamoja naye, kwa kumpatia Roho Mtakatifu. Anasema, “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Luka 11:13).
Bwana ametuagiza kumwita Mungu Baba yetu, kumchukulia kuwa chemchemi ya upendo wa baba, chanzo cha upendo ule ambao umekuwa ukitiririka toka karne hadi karne kupitia katika mfereji wa moyo wa mwanadamu. Huruma zote, masikitiko, na upendo ambao umedhihirishwa katika dunia umetoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na, ukilinganisha na upendo ule unaokaa katika moyo wake, ni kama chemchemi ilivyo kwa bahari.
Upendo wake milele unatiririka ili kumfanya aliye dhaifu kuwa na nguvu, kumfanya anayezimia moyo kuwa imara, na kumpatia moyo wa kuthubutu yule mwenye kusitasita. Mungu hutenda kazi kupitia kwa Kristo, na mwanadamu anaweza kuja kwa Baba kwa jina la Mwana. Sayansi yetu na wimbo wetu ni “Sikiliza kile ambacho Bwana ametenda kwa ajili ya roho yangu.” - Signs of the Times, March 5, 1896.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon