KUTUMAINIA NURU YAKE!

Image may contain: text






Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, naam, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Zaburi 119:34.

Kwenye eneo lote la ufunuo kumeenea chemchemi za furaha za ukweli, amani na furaha ya kimbingu. Chemchemi hizi za furaha ni rahisi kufikiwa na kila mtafutaji. Maneno ya uvuvio, yakitafakariwa moyoni, yatakuwa kama vijito vinavyotiririka kutoka kwenye mto wa maji ya uzima. Mwokozi wetu aliomba kwamba akili za wafuasi wake zipate kufunguliwa ili zielewe Maandiko. Wakati wowote tunapojifunza Biblia kwa moyo wenye maombi, Roho Mtakatifu huwa karibu akitufungulia maana ya maneno tunayoyasoma. Mtu ambaye akili yake imeangazwa kutokana na kufunguliwa kwa Neno la Mungu kwa ufahamu wake, hatajisikia tu kulazimika kutafuta kwa dhati kulielewa Neno hilo, bali pia atapata kuwa na uelewa ulio bora zaidi wa sayansi. Atajisikia kwamba ameitwa kwa ajili ya wito mkuu katika Kristo Yesu.

Kadiri mtu anavyokuwa karibu na Chanzo cha ufahamu wote na hekima yote, ndivyo atakavyozidi kujisikia kwamba ni lazima aendelee kupata mafanikio ya kiakili na ya kiroho. Kufungua Neno la Mungu daima kunafuatiwa na kufungua na kuimarishwa uwezo wa mtu isivyo kawaida; kwani kuingizwa kwa maneno yake kunaleta nuru. Kwa kutafakari ukweli huu mkuu, akili huinuliwa, kupenda kwake kunasafishwa na kutakaswa; kwani Roho wa Mungu, kupitia kwa ukweli wa Mungu, huhuisha uwezo wa kiroho usio na uhai na kuvutia roho kuelekea mbinguni.

Kisha chukua Biblia yako na ujiweke mwenyewe mbele za Baba wa mbinguni, ukisema, “Niangazie; nifundishe kilicho kweli.” Bwana ataheshimu ombi lako naye Roho Mtakatifu ataweka ukweli kwenye moyo wako. Unapochunguza Maandiko wewe mwenyewe, utaimarika katika imani. Ni jambo la muhimu sana kwamba udumu kuchunguza Maandiko, ukihifadhi ukweli wa Mungu akilini. Unaweza kutenganishwa na ushirika wa Wakristo na kuwekwa mahali ambapo hutakuwa na fursa ya kukutana na watoto wa Mungu. Utahitaji kuwa na hazina ya Neno la Mungu ikiwa imefichwa moyoni mwako, ili wakati upinzani unapokujia, uweze kuleta kila kitu kwenye vipimo vya Maandiko. – Bible Echo, Okt. 15, 1892.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.