
Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. Zaburi 119:18.
Sehemu nyingi za Maandiko ambazo wasomi huzisema kuwa ni mafumbo, au huzipitia kana kwamba sio za muhimu, zimejazwa kwa faraja na maelekezo kwake ambaye amefundisha kwenye shule ya Kristo. Sababu moja inayofanya wanateolojia kutokuwa na uelewa dhahiri zaidi wa Neno la Mungu ni kwamba, wao hufunga macho yao wasione ukweli ambao hawatamani kuutenda. Uelewa wa ukweli wa Biblia hautegemei zaidi uwezo wa kiakili unaotumika katika uchunguzi kama unavyotegemea kufanya kazi kwa lengo moja, shauku ya dhati ya uadilifu.
Kamwe Biblia isijifunzwe bila maombi. Ni Roho Mtakatifu pekee atakayetusababisha tujisikie umuhimu wa mambo yale yaliyo rahisi kueleweka, au kutuzuia tusilazimishe ukweli ambao ni mgumu kueleweka. Ni kazi ya Roho Mtakatifu kuandaa moyo ili upate kuelewa Neno la Mungu ili tupate kuchangamshwa na uzuri wake, kuaswa na maonyo yake, au kuamshwa na kutiwa nguvu na ahadi zake. Inatupasa kufanya ombi la mtunga zaburi kuwa letu: “Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako.”
Mara kwa mara majaribu huonekana kutopingika kwa sababu, kwa kupuuzia maombi na kujifunza Biblia, anayejaribiwa hawezi kukumbuka kwa haraka ahadi za Mungu na kukabiliana na Shetani kwa silaha za Maandiko. Lakini malaika huwazungukia wale walio tayari kufundishwa mambo ya kimbingu; na katika wakati huu wa hitaji kuu watawakumbusha ukweli halisi unaohitajika. Kwa namna hiyo, “yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana” (Isaya 59:19).
Yesu aliwaahidi wanafunzi wake: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:26). Lakini mafundisho ya Kristo ni lazima yawe kwanza yamehifadhiwa akilini ili Roho wa Mungu ayalete katika kumbukumbu zetu wakati wa hatari. Daudi alisema, “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi (Zaburi 119:11). – The Great Contorversy, kur. 599, 600.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon