
Ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu.
1Wakorintho 2:5 -7.
Mnakubalika katika yeye Apendwaye. Nimekuwa na shauku kubwa sana kwamba mpate kukamilisha tabia ya Kikristo, siyo kwa nguvu zenu wenyewe, bali katika nguvu na sifa na haki ya Kristo. Msaada wa Roho Mtakatifu ulikuwa zawadi kubwa zaidi ambayo Mungu alitoa kwa mwanadamu mwenye kikomo. Karama hii ni bure kwa wote na katika hii hakuna mahesabu; kipaji hiki kwa namna ya pekee kilisimama kuwa kielelezo cha kutawadhwa kwa Mwana pekee wa Mungu katika ufalme wake wa upatanishi. Katika hii, karama ya Mfariji, Bwana Mungu wa mbinguni anamwonesha mwanadamu upatanisho kamili ambao aliufanya kati yake mwenyewe na watu. Mtume anasema, “Tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu” (Waebrania 6:19, 20).
Je?, Mungu hakusema kwamba atawapatia Roho Mtakatifu wale wamwombao? Na huyu Roho siye Kiongozi halisi, wa kweli, wa hakika? Baadhi ya watu wanaonekana kuogopa kuamini kile Mungu alichosema hasa, kana kwamba hilo lingekuwa hali ya kuonesha kiburi. Hawa huomba Bwana atufundishe na wakati huo huo wakiogopa kusadiki neno la Mungu na kuamini kwamba tumefundishwa naye. Kadiri tuwezavyo kumjia Baba yetu wa mbinguni kwa unyenyekevu na kwa roho iliyo tayari kufundishwa, tukiwa na nia na wenye shauku ya kujifunza, kwanini tutilie mashaka utimilifu wa ahadi aliyoitoa Mungu mwenyewe? Hupaswi kumtilia mashaka hata kidogo na kwa namna hiyo kumvunjia heshima.
Unapokuwa umetafuta kujua mapenzi yake, sehemu yako katika kutenda pamoja na Mungu ni kuamini kwamba utaongozwa na kuelekezwa na kubarikiwa katika kufanya mapenzi yake. Tunaweza kutojitumainia sisi wenyewe ili tusipotoshe tafsiri ya mafundisho yake, lakini hebu hata hili lifanye kuwa suala la kuombea nawe umtumainie yeye, dumu kumtumainia kikamilifu, kwamba Roho wake Mtakatifu akuongoze kufasiri kwa usahihi mipango yake na kazi za busara yake. – Manuscript Releases, vol. 6, uk. 223, 224.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon