
Asili ya Easter
Rejea nukuu zifuatazo.
“Neno la kingeleza Easter na la kijerumani Ostere yote yanatokana na asili moja (Eostur, astur, Ostara, Ostar), ambalo kwa Wanorwei humaanisha msimu wa kuinuka (kukua) jua, msimu wa kuzaliwa upya. Neno hilo lilitumiwa na mababu zetu kuteua sikukuu ya maisha mapya katika majira ya vuli. Mzizi huo huo unaonekana kwa ajili ya mahali ambapo jua huchomoza (East, Ost). Neno Easter, harafu, kwa asili linamaanisha maadhimisho ya jua katika majira ya vuli (spring sun) ambayo yanazaliwa katika mashariki na kuleta maisha mapya juu ya nchi. Ishara hii ilihamishwa kuwa maana isiyo ya kawaida ya Pasaka (Easter) yetu, kwa maisha mapya ya Kristo aliyefufuka, aliye nuru ya milele isiyoumbwa. Kulingana na kifungu katika maandishi ya mtakatifu Bede Mpendwa, neno Easter mara kwa mara limeelezewa kama jina la mungu mke wa waingereza (Eostre)…...” –Francis X. Weiser,Handbook of Christian Feasts and Customs (New York: Harcourt, Brace & World, Inc., 1958), p. 211. Copyright 1952 by Francis X. Weiser.…Ostara.
“(Kama machi 21 lakini tarehe zinaweza kutofautiana kama siku mbili) pia inajulikana kama; Ikwinoksi ya majira ya vuli, Ostara, Alban Eiler, Esther, Eostre, Ostarun, startag’, Eastre, Eoastrae, Oestre Siku ya kwanza ya kweli ya kuchipuka. Mchana na usiku sasa zote ziko sawa katika urefu kama mungu kijana anavyoendelea kukomaa na kukua. Tunaanza kuona mashina ya ukuaji mapya na machipukizi yanayopanuka katika miti. Nishati inajenga kadri siku zinavyozidi kuwa joto pamoja na ahadi. Unaweza; unaweza kuiita Easter Sisi tunaiita Ostara [1 assays -56, 869 inasomeka]–Unaiita Easter (pasaka), sisi tunaiita Ostara na Peg Aloi. Jaribu hii wakati mwingine pamoja na watoto wako au mpwa kijana, mpya au binamu: Siku ya Ikwinoksi ya majira vuli muda mfupi tu kabla ya wakati halisi wa Ikwinoksi.” –-The Witches VoiceThe 8 Pagan Holidays
“Je nini maana ya neno Easter lenyewe? Siyo jina la Kikristo. Linachukua asili ya Ukalidayo katika paji lake la uso kabisa. Easter sio kitu kingine zaidi kuliko Astarte, moja ya majina ya Beltis, malikia wa mbinguni, ambaye jina lake, kama lilivyotamkwa na watu wa Ninawi, alikuwa kwa dhahiri anatambulikana hivyo sasa katika matumizi ya kawaida katika nchi hii. Jina hilo, kama Lyard alivyolipata katika makaburi ya Ashuru ni Ishtar.” –The Two Babylons, na Alexander Hislop, kilichochapishwa 1943 na 1959 katika U.S. na Loizeaux Brothers, Neptune, New Jersey, page 103.
“Hakuna dalili ya uadhimishaji wa sikukuu ya (Easter) katika Agano Jipya au katika maandiko ya mababa wa kanisa la mitume.” Mwanahistoria wa kanisa, Socrates amenukuliwa katika makala hiyo hiyo kama anavyoonyesha kwamba Bwana wala mitume wake hawakujiingiza katika kutunza siku hii. Anasema, “Mitume walikuwa hawana wazo la kuteua siku za sikukuu, lakini la kukuza maisha yasiyo na mawaa na ucha Mungu.” Anahusisha maadhimisho ya Pasaka na kanisa kwa kuendeleza matumizi ya zamani, “vile vile kama desturi zingine ambazo zimeanzishwa.” Wanamatengenezo wa kanisa la mwanzo kama vile Calvin na Knox walipinga kwa nguvu dhidi ya Pasaka ya Katholiki (Easter) kwa sababu ya asili yake ni ya kipagani. Uadhimishaji wa siku hiyo haukusherehekewa sana katika Marekani mpaka baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe. (Easter: Its Story and Meaning by Alan Watts; Babylon, Mystery Religion, Ralph Woodrow;Calvin Tracts; Knox’s History) –Encyclopedia Britannica, article “Easter”
“Wakati Waprotestanti walipokuja amerika ya kaskazini, waliiangalia sherehe ya Pasaka–na sherehe ya Krismasi–kwa kuzituhumu. Walijua kwamba wapagani walisherekea kurudi kwa majira ya vuli kwa muda mrefu kabla ya Wakristo kusherehekea Pasaka (Easter)…kwa miaka mbali mbali ya mwanzo ya maisha ya Ulaya katika Amerika ya kasikazini, walikuwa tu wachache, wengi wao katika upande wa kusini, waliipa kipaumbele sana Pasaka” Siyo mpaka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoisha Waamerika wakaanza kusherekea sikukuu hii; Pasaka mwanzo ilikuwa desturi ya Marekani katika miaka ya 1870. Chakukumbukwa! ni koloni 13 za awali za amerika zilianza kama taifa la “Kikristo” kwa kilio cha “Hakuna Mfalme ila Yesu!” Taifa halikuadhimisha Pasaka ndani ya karne nzima ya kuanzishwa kwake. Je nini kilitokea kulibadilisha hili?” -A Children’s book about the holiday, Easter Parade: Welocome Sweet Spring Time!, na Steve Englehart, p 4-5
Wana wa Israeli pia waliangukia katika ibaada hizi za kipagani za “malkia wa mbinguni,” na walioka mikate kwajili ya kumtukuza.
Yeremia 7:18 “Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.”
“Ishtar alikuwa mama mkuu, mungu mke wa uzaaji na malikia wa mbinguni.” -Microsoft Encarta Multimedia Enyclopedia.
Harafu angalia kwa makini Ishtar “malikia wa mbinguni” ndiye yule yule Beltis, au Semiramis, au Astarte mungu mke wa Ashuru ambaye jina lake ni” (“Easter”). Jina jingine la mungu mke huyo ni “Asht-tart” ambalo kwa kiebrania ni “Ashtoreth.” Ibada ya Ashtorethi mfalme Sulemani aliingiza katika Israeli wakati amemwasi Bwana, na kusababisha Israeli imwache Bwana na kuleteleza uharibifu wa kitaifa.
kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake. (1 Wafalme 11:33). Leo pia ibada hii ya Ashtorethi imeingizwa kanisani na mapapa na kuleta uharibifu wa Kanisa la Kristo, Mungu hatanyamaza juu ya hili, bali atachukua hatua kama alivyochukua hatua kwa Israeli ya zamani. Jipone nafsi kwa kuachana na upagani huu.
“Nini maana ya neno Easter lenyewe? Siyo jina la Kikristo. Linachukua asili ya ukalidayo katika paji lake la uso kabisa. Easter siyo kitu kingine zaidi ya Astarte, moja ya majina ya Beltis, malikia wa mbinguni… mungu mke wa Ashuru, au Astarte, anatambulika kama Semiramis. By Athenagoras (Legatio, vol. ii. p. 179), na [by] Lucian (De Dea Syria, vol. iii. p. 382)…sasa, hakuna jina linaloweza kwa hakika zaidi kutoa picha ya sifa ya Semiramis kama malkia wa Babeli, kuliko jina la ‘Asht-tart,’ kwa maana hilo humaanisha “Mwanamke yule aliyefanya minara”…Ashturit, harafu…ni kwa wazi jina hilo hilo kwa kiebrania ni ‘Ashtoreth.'” -Alexander Hislops, The Two Babylons, pp 103, 307-308).
Majina yote haya Beltis, Semiramis, Easter(Pasaka), Astarte, na majina mengine mengi tuliyoona huko nyuma ni majina ya mungu mke ambaye ni malkia wa mbinguni, na jina lake hili “Asht-tart” kwa kiebrania ni “Ashtoreth”. Na katika Biblia tunaona Mungu aliwakataza wana wa Israeli kuwa na sikukuu hizi za maashtorethi, au Easter
Waamuzi 3:11-13 “Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali…wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote…Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.”
1Samweli 7:3-4 “Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katikaMatendo 2:42 “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.”
Wakatoliki waliingiza sherehe ya pasaka wakidai ni kwa ajili ya kuadhimisha ufufuo wa Yesu Kristo. Lakini kibiblia Wakristo huadhimisha Kifo na Ufufuo wa Yesu kwa njia ya ubatizo.
Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake….Warumi 6:3-5
Wakatoliki hudai kwamba ule mkate ni mwili halisi wa Yesu, na ile divai ni damu halisi kabisa ya Yesu, lakini huo sio ukweli. Mkate na divai ni viwakilishi tu, na sio vitu halisi. Kwa sababu kama ni hivyo Kristo pia katika Maandiko huwakirishwa kama mzabibu. Je Kristo ni mzabibu halisi kweli? Pia huwakirishwa kama kondoo, Je Yeye ni kondoo halisi kweli? Kulingana na kanisa Katoliki Yesu ni mti wa mzabibu, au kondoo halisi. Yeyote anayemruhusu Roho wa Mungu kumfundisha ataona wazi kwa macho ya kiroho kuwa huo si ukweli.
1Wakorinto 10:18-21 “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.”
Kikombe au meza ya Bwana ni Agizo la Kristo la kumega mkate na kunywa divai.
Kikombe au meza ya shetani ni agizo la kanisa Katoliki la kuadhimisha Pasaka(Easter) sikukuu waliyosherehekea wapagani zamani kwa kuheshimu “ufufuo” wa jua, tamuzi au baali.
Ndugu hatuwezi kushiriki katika meza ya Bwana, na meza ya mashetani.
1Wakorintho 10:22 “Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?”
Sikuhukumu bali nimebainisha historia ya Ukristo, ni uhuru wako kukubali au kukataa. Na ni haki yetu na wajibu wetu kuichunguza kweli ya wakati huu. Na tunapojifunza ya kwamba hiyo ndiyo kweli, basi, na tuipokee na kuitii. Amen
Mungu akubariki kwa kufuatilia na kusoma.
1 comments:
Write commentsNaam, imeandikwa yohana 8:32,mtaijua kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru... Ingawaje wakristo wako na bible lakini hawaisomi bible,, biblia ni pumzi ya MUNGU (neno la MUNGU). naam, na yote yasiyo andikwa humo ni maneno ya wanadam hayafai kufatwa kabisa. Lakini je, jamii itakuelewa vipi kama baba yako wa kiroho yu miongoni mwa watu wanao sherehekea hizo paganic holiday? Lakini mimi najua neno moja tu yakwamba nitaijua kweli nayo hiyo itaniweka huru katika yeye anitiaye nguvu. Amen amen,
ReplyEmoticonEmoticon