AMRI KUMI KATIKA AGANO JIPYA



No automatic alt text available.







1.Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; lakini kwetu sisi MUNGU NI MMOJA TU, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake…..1 Wakorintho 8:5,6

2.WALA MSIWE WAABUDU SANAMU… 1 Wakorintho 10:7
Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.1 Wakorintho 10:14. Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. 1 Yohana 5:21. Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.Matendo ya Mitume 17:16

3.JINA LA MUNGU LISITUKANWE... 1 Timotheo 6:1
lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake…Mathayo 5:34,35

4. Akawaambia, SABATO ILIFANYIKA KWA AJILI YA MWANADAMU, Si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi MWANA WA ADAMU NDIYE BWANA WA SABATO PIA. Marko 2:27,28. Basi, IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.Waebrania 4:9. Mathayo 12:12.. Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato. Mathayo 24:20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.Matendo ya Mitume 17:2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,

5. WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO.. Mathayo 19:19
Waefeso 6:1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

6. .USIUE. Marko 10:19
1 Petro 4:15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji….1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.

7. USIZINI. Marko 10:19

8. .USIIBE. Marko 10:19
Waefeso 4:28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

9. USISHUHUDIE UONGO. Marko 10:19
Waefeso 4:25 Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake. Wakolosai 3:9 Msiambiane uongo…

10. USITAMANI. Warumi 13:9
Wagalatia 5:14 ..Umpende jirani yako kama nafsi yako.

Wale wanaodai kuwa Amri kumi ziligongomelewa msalabani na wajitokeze.

WITO WA BWANA YESU:
Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Yohana 15:10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

WITO WA MITUME:
1 Wakorintho 7:19 Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.

2 Yohana 1:6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. 1 Yohana 2:3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

1 Yohana 2:4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.

Yakobo 2:12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.