KUTOKA PASAKA HADI EASTER. (4)


No automatic alt text available.







Maana ya jina Easter.

Jina awali la kingereza linalotumika kuielezea Pasaka hii iliyoanzishwa na kanisa Katoliki ni “Easter” ambalo ukitoa herufi 2 mwishoni linamaanisha “mashariki.” Jina hili lilikuwa jina la miungu ya kipagani, tena lilitumika kuwakilisha sikukuu za kipagani za Ikwinoksi ya majira ya vuli (Machi 21 na Aprili 25).
Jina Easter ni sawa na jina “Astarte” mungu mke wa Ashuru anayejulikana kama “malikia wa mbinguni” (Angalia neno “Easter” katika Dictionary ya English to English).

“Mwishoni mwa majira ya baridi, msimu hubadilika kwa sababu dunia huinama kama inavyozunguka kwenye mhimili wake. Majira ya vuli hufika wakati jua liko juu ya ikweta. Katika siku ya kwanza ya majira ya vuli, inayojulikana kama Ikwinoksi (majira huwa sawa usiku), vyote usiku na mchana vinakuwa sawa urefu wa masaa 12. Ambapo humaanisha kwamba siku ndefu za majira ya baridi zimeisha, na kwamba jua tena linaanza kuchukua udhibiti. Wakati huu ulikuwa ni maadhimisho na sikukuu kuwashukuru miungu ya kipagani. Taratibu hizi za dini ya kizamani zilikuwa ni sikukuu ya uzaaji, waliyoiazimisha katika tumaini kwamba miungu wangewabariki kwa makundi yanayozaa na mashamba. Kafara za mnyama na mtoto zilitolewa kwa miungu ili kuipokea neema hii.

“Mpendwa Bede, mwanahistoria wa Kikristo wa karne ya nane, alionyesha kuwa jina Easter lilitokana na sikukuu ya “Oestre” (“Ostere,” “Ostara”), mungu mke wa Waingereza wa majira ya vuli na uzaaji. Kulikuwa pia na mungu mke wa Teutonic (Kijerumani) aliyejulikana kama “Eostre” (pia alijulikana kama “Eastre” “Estre”), ambaye alikuwa ni mungu mke wa giza na nuru, uzaaji na majira ya vuli. Ni kutokana na miungu hawa ambapo jina Easter (Pasaka) lilianzishwa. Sikukuu ya heshima yake ilifanyika wakati wa Ikwinoksi.” -Controlled by the Callendar, p 42.

Asili ya mayai na sungura katika Easter

Tamuzi mtoto wa Easter(Semiramis) alipenda kufuga Sungura, kwa wapagani kwa kukumbuka kifo chake kilichotokana na Nguruwe mwitu wakati anawinda, walitumiana kadi au sanamu zenye alama ya Sungura kwa kumbukumbu ya mungu wao, na ile siku aliyokufa hawakula nyama. Na siku ya ufufuko wake walikula sana Nguruwe sana baada ya maombolezo ya kujipaka majivu, walikula Nguruwe siku ya sherehe (jumapili) kama ishara ya kulipiza kisasi kwa muuaji wa Mungu wao. Siku hiyo ya sherehe walishika matawi mabichi kama ishara ya ufufuo wa Tamuzi, maana waliamini damu yake ilirukia majani mabichi wakati anauliwa na Nguruwe, tangu hapo sehemu za majani mabichi zilikuwa wakfu kwa ibada za kipagani. [1 Wafalme 14:23; 2 Nyakati 28:4 ]. Na mama yake Tamuzi wapagani waliamini alitokea mwezini kama yai, na akaangukia mto flati na kujiangua, kwahiyo yai lilimwakilisha yeye na kuitwa Ishta egg, na sherehe ya mwanae ilibeba jina lake. Tamuzi alikuwa ana majina mbalimbali kulingana na kabila, Wamisri walimwita Horus, Wahindi walimwita Krishna, Wagiriki walimwita Cupid. Hii Imani ya kipagani iliwai kuingia Israel na kusababisha waadhibiwe kwenda utumwani, Biblia inatupa rejea hii ‘’Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia TAMUZI. Akaniambia, Mwanadamu umeyaona haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo.’’,Ezekieli 8:14,15.

Inaendelea....
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.