KUTOKA PASAKA HADI EASTER. (3)


No automatic alt text available.







Kipindi cha Kwaresima.

Kwaresima ni kipindi cha kufunga na toba cha siku 40 kinachoanza katika siku ya “Jumatano ya majivu” na kinaendelea mpaka siku ya pasaka. Kwaresima haionekani popote katika Biblia, hata Yesu na mitume walipomega mkate walikuwa hawajawahi kufunga kwanza siku-40 za Kwaresima. Historia inasema…

“Lakini ungetakiwa kujua, kwamba kadri kanisa la awali lilivyoshikilia ukamilifu bila kuharibika, uadhimishaji wa Kwaresima haukuwepo.” -Johannes Cassianus, First Conference Abbot Theonas, chapter 30.

Lakini baada ya mitume na Wakristo wote wa mwanzo kufaliki, kanisa Katoliki liliingiza uadhimishaji wa kipindi cha Kwaresima na kudai kwamba kinawakilisha siku-40 alizofunga Yesu jangwani. Lakini kwa vyovyote, Kwaresima ya siku-40 za kufunga kabla ya pasaka, ilisherehekewa na wapagani wa zamani kwa ajili ya jua. Historia inatuambia…

“Siku-arobaini za kipindi cha toba ziliazimishwa zamani katika kutoa heshima kwa miungu ya kipagani Osiris, Adonis na Tamuzi” -John Landseer, Sabaean Researches, pp. 111, 112.

“Siku arobaini za toba za Kwaresima moja kwa moja zilikopwa kutoka kwa waabudu miungu ya Babeli. Kwaresima kama hiyo ya siku arobaini, katika majira ya vuli ya mwaka, bado inaadhimishwa na wa-Yezidis au wapagani waabudu-shetani wa Koordistan, ambao wameirithi kutoka kwa walimu wao wa mwanzo, wababeli. Kwaresima kama hiyo ya siku arobaini ilifanywa katika majira ya vuli na wamexico wapagani…Kwaresima kama hiyo ya siku arobaini iliadhimishwa huko Misri.” -Alexander Hislops, The Two Babylons, p 104-105.

“Kipindi cha siku arobaini za toba na sala ambacho huanzia siku ya Jumatano ya majivu na huandaa kwa ajili ya maadhimisho ya pasaka. Ingawa awali kilidumu chini ya wiki moja, wakati wa karne ya saba ikawa inawakirisha siku arobaini alizotumia Kristo jangwani. Wakati kilipoanzishwa mwanzo na kanisa Katoliki, baadhi ya watu walifanya muda mwingi pamoja na ubaguzi wa Jumapili. Hivi sasa wengi “huacha” siku moja au mbili wakati wa kipindi hiki.

“Neno “Kwaresima” (“Lent”) linatoka katika kingeleza cha zamani “Lencten” ambalo humaanisha “Majira ya vuli.” Liliundwa na kanisa Katoliki kati ya mwaka 525 AD, chini ya uongozi wa padri Dionysus mdogo, Kwaresima ni kipindi cha siku-40 kutoka Jumatano ya majivu hadi Pasaka, ambacho huwekwa pembeni kwa ajili ya kufunga na kutafuta toba. Maadhimisho hayo hayapatikani katika Biblia, hivyo hayakutambuliwa na Yesu, mitume, au kanisa la Kikristo la mwanzo. Hata hivyo, siku za leo, kwa kawaida kinamaanisha “kuacha” kitu fulani, kwa kawaida baadhi ya tabia mbaya, au hata kufuta kabisa, ili kumpendeza Mungu. Kipindi hiki…kwa hakika asili yake ni Babeli, kama asili ya siku ya mwaka ambayo iliheshimu kifo na ufufuo wa Tamuzi; na badaye iliadhimishwa huko Misri kumheshimu Osiris, mwana wa Isis, ambaye alikuwa marudio ya Tamuzi.

“Wakati Nimrodi alipokufa, alifanywa mungu jua, harafu Semiramis [mke wake] alikuwa na mwana wa haramu aliyeitwa Tamuzi, ambaye yeye alidai kuwa ni mwana wa Nimrodi. Alisema kwamba alikuwa “mzao aliyeahidiwa wa mwanamke” (Mwanzo 3:15) na akataka kwamba wote yaani yeye na Tamuzi waabudiwe. Tamuzi akafanyiwa ishara ya ndama wa dhahabu. Semiramis akajulikana kama “malikia wa mbinguni,” na alikuwa ishara ya miungu wa kike wote wa kipagani waliokuja baadae. Mwakilishi wake anaweza kuonekana katika ibaada ya Maria ya kanisa la Romani Katoliki ambaye huitwa “mama wa kanisa” “malikia wa mbingu na nchi,” na “malikia wa ulimwengu.” Majina haya hayawezi kurejea kwa Maria, Mama wa Yesu, kwa sababu hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia inapozungumzia mamlaka ya Maria kwa jinsi hiyo.


“Kulingana na desturi za Babeli wakati Tamuzi alipouwawa, mama yake alilia sana, ili Tamuzi arudi tena kuwa hai. Udhihirisho wa hili ilikuwa ni kuzaliwa upya na kustawi kwa mimea yote katika majira ya vuli, ambayo yalikuja kuashiria kufufuka kwake, na hii ndiyo sababu Tamuzi anaheshimiwa katika majira ya vuli. Kitu kile kile ni hadithi ya zamani katika maandiko ya Semiramis, huko Mesopotamia, ambayo yalisema kuwa Tamuzi alimwoa mungu mke Inana (Ishtar) “mama mungu mke.” Wakati Tamuzi alipouwawa, mama yake alishindwa na huzuni, kiasi kwamba alimfuata kuzimu, na kwa kutokuwepo kwake, nchi ikaanza kufa, mazao yakasimama kukua, na wanyama wakasimama kupanda. Ea, mungu wa maji na hekima, alituma ujumbe kwamba Inanna arudishwe tena. Mjumbe huyu aliwanyunyizia wote Inanna na Tamuzi kwa maji ya uhai, na walipewa nguvu za kurudi kwenye mwanga wa jua kwa miezi sita ya mwaka. Harafu Tamuzi angerudi tena chini kuzimu, na hivyo kumsababisha Inanna kumfuata yeye, na tena, Ea angewarejesha wote.

“Ezekieli 8:12-14 inazungumzia kuhusu wanawake wakimlilia Tamuzi na hii ni hakika inarejea kwa siku-40 za kipindi cha Kwaresima.” -Controlled by the Calendar, p 46, 47.

Inaendelea...
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.