HATARI KUU I MBELE YETU.

"Pambano kuu la mwisho li mbele yetu, lakini msaaada utakuja kwa wote wanaompenda Mungu na kutii sheria yake, na dunia, naam dunia yote, itaangazwa kwa utukufu wa Mungu.
'Malaika mwingine atashuka kutoka mbinguni. 
Malaika huyu huwakilisha utoaji wa kilio kikuu, ambacho kitatoka kwa wale wanaojiandaa kulia kwa sauti kuu, kwa sauti ya nguvu, 
"Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya Mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza"
(Ufunuo 18:1,2).


"Tunao ujumbe wa mtihani wa kutoa, na nimeagizwa kusema kwa watu wetu, 'Unganeni, unganeni.' Lakini haitupaswi kuungana na wale wanaotoka kwenye imani, wakifuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. 
kwa mioyo yetu safi na ukweli na utulivu, tunapaswa kwenda mbele kutangaza ujumbe, bila kuwajali wale wanaopotosha kutoka kutoka kwenye kweli."
Selected Messages, kitabu cha 3, uk. 412
(Manuscript 31, 1906).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.