YESU ATAWALAPO HAKUNA HOFU ITAKAYOKUTISHA.



Umewahi kujiuliza wimbo usemao "Ni Salama Rohoni Mwangu" mtunzi aliyeutunga alikuwa ktk wakati gani?! 

Ebu sikia kisa kizuri hiki cha kuvutia cha mtunzi wa wimbo huu, wimbo huu wa "Ni Salama Rohoni Mwangu" Mtunzi wa wimbo huu anaitwa Horatio Spafford, wakati akiwa anasafiri toka Marekani kwenda Uingereza akiwa na mabinti zake wanne walipata ajali na mabinti zake walikufa maji yeye alipona hapo ndipo alipotunga wimbo "Ni Salama Rohoni Mwangu" hii ilikuwa ni mnamo mwaka 1883.

Mtu huyu alikuwa na tumaini la ajabu sana kwa Mungu wake, mara nyingi tunapopitia shida na majaribu mbalimbali twapata wakati mgumu sana mioyo haitulii majonzi hututawala na roho za manung'uniko ututawala, wakati mwingine tunamlaani Mungu kana kwamba ameshindwa kutuokoa ama kuzuia yote mabaya yasitupate.

Oooh mpendwa jaribu kuifundisha akili yako kushukuru kwa kila jambo, Kristo atawalapo moyo uwa na amani Kama Ayubu alivyomtukuza Mungu ktk shida zote alizopitia, wakati mwingine Mungu huyaruhusu kutufundisha hivyo basi twapaswa kumshukuru Mungu kwa yote yatupatayo!!!!!

Furahini siku zote; Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu ktk Kristo Yesu. 1Wathesalonike 5:16-18.

Ndugu mpendwa mtwike Yesu fadhaa zako naye atakupatia amani moyoni ikiwa dunia igeukie mawimbi ya bahari yachafuke, Marafiki wakutenge, hata na ndugu pia usiangaike kujilaani, mtwike Yesu fadhaa zako.
Moyo ule unaomtumaini Kristo ujazwa amani na furaha maana Kristo uutawala na kuongoza yote tujifunze kumwangalia Kristo wakati wote naye atatuongoza mpaka kwenye bandari salama..... Mbarikiwe!!!!


Image may contain: cloud, sky, text, nature and outdoor
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.