KUCHAGUA MKE



Hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao; bali enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke. Mwanzo 24:3,4.


Imani ya kila siku ya Ibrahimu katika Mungu na kujisalimisha kwa mapenzi yake viliakisiwa katika tabia ya Isaka; lakini mapenzi ya kijana yalikuwa na nguvu na alikuwa mpole na mwenye silika ya kukubali. Kama angeunganika na mtu ambaye hakumcha Mungu, angekuwa kwenye hatari ya kuacha kanuni kwa sababu ya kutaka mapatano.

Mawazoni mwa Ibrahimu, uchaguzi wa mke kwa ajili ya mwana wake lilikuwa suala la muhimu sana; alikuwa na shauku ya kuhakikisha anaoa mtu ambaye asingemwondoa kwa Mungu….

Ibrahimu alikuwa ameona matokeo ya kuoana kati ya wale waliomcha Mungu na wale ambao hawakumcha, kutokea siku za Kaini hadi wakati wake. Matokeo ya ndoa yake na Hajiri na ya muunganiko wa ndoa za Ishmaeli na Lutu zote zilikuwa mbele yake.

Upungufu wa imani kwa upande wa Ibrahimu na Sara kulileta matokeo ya kuzaliwa kwa Ishmaeli, kuchanganywa kwa mbegu takatifu na ya waovu.

Mvuto wa baba kwa mwana wake ulizuiwa na ule wa ndugu za mama waliokuwa waabudu sanamu na ule wa muunganiko wa Ishmaeli na wanawake wa kipagani…

Mke wa Lutu alikuwa mbinafsi, mwanamke asiye na dini na mvuto wake ulitumika katika kuwatenganisha mume wake na Ibrahimu. Isingekuwa kwa sababu yake, Lutu asingebaki Sodoma, akinyimwa ushauri wa hekima wa yule mzee mcha – Mungu…

Hakuna mtu anayemcha Mungu ambaye hawezi kuwa hatarini anapojiunganisha na mtu asiyemcha. “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” (Amosi 3:3).

Furaha na mafanikio ya uhusiano wa ndoa yanategemea umoja wa wale wahusika; lakini kati ya muumini na asiyeamini ipo tofauti kubwa katika utashi, mielekeo na makusudio. Hawa wanakuwa wakitumikia mabwana wawili, ambao kati yao haiwezekani kuwepo na mapatano. Hata kama mmoja atakuwa na kanuni safi na sahihi kiasi gani, mvuto wa mwenzi asiyeamini utakuwa na kawaida ya kuongoza kuelekea mbali na Mungu…

Maelekezo ya Bwana ni, “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini” (2 Wakorintho 6:14, 17, 18).


Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi Maombolezo 3:22-23

Image may contain: 2 people, people sitting


Previous
Next Post »
Powered by Blogger.