Wakati wa hari u mbele yetu. Kila mmoja anayejua kweli angeamka, na kuuweka mwili wake, mawazo, moyo na roho chini ya uongozi wa Mungu. Adui yu katika njia yetu. yatupasa tukeshe tukimpinga. Yatupasa tuvae silaha zote za Mungu. Yatupasa tufuate maagizo tuliyopewa kwa njia ya Roho ya Unabii. Yatupasa tuutii na kuupenda ukweli wa wakati huu. Kwa njia hii tutaokolewa katika kuupokea udanganyifu mkubwa. Ambao Mungu amezungumza nasi kwa njia ya maonyo ya kanisa, na kwa njia ya vitabu ambavyo vilisaidia kuufanya waazi wajibu wetu wa sasa na hali ambayo tungekuwa nayo.
Onyo ambalo limetolewa mstari kwa mstari, amri kwa amri, lingefuatwa. Tusipojali, tutatoa udhuru gani? (Kutayarisha Njia sehemu ya pili, uk, 64).

EmoticonEmoticon