KIONGOZI PEKEE.

Image may contain: 1 person




"Neno lako ni taa ya miguu yangu, 
Na mwanga wa njia yangu."
Zaburi 119:105. 

Ni wajibu wa kwanza na wajuu kabisa wa kila mwanadamu mwenye akili kujifunza kile ambacho ni kweli kutoka kwenye Maandiko, na kisha kutembea katika nuru na kuwatia moyo wengine kufuata mfano wake.
Tunapaswa kujifunza Biblia kwa makini na kwa bidii siku kwa siku, tukipima kila wazo na kulinganisha andiko kwa andiko. Kwa msaada wa Uungu tunaweza kujenga mawazo yetu kwa ajili yetu wenyewe wakati tutakapopaswa kujibu kwa ajili yetu wenyewe mbele za Mungu.
(Pambano Kuu, uk. 496).

Moyo (akili) umeumbwa kwa namna ambayo unapaswa kushughulishwa na mema au maovu. Kwa kawaida unapokuwa katika usawa wake wa chini ni kwa sababu unaachiwa kushugulika na mambo ya kawaida.
. . . Mwanadamu anao uwezo wa kuratibu na kutawala utendaji wa akili yake, na kutoa mwelekeo wa mtiririko wa mawazo yake. Lakini jambo hilo huhitaji juhudi kubwa kuliko ile tunayoweza kuitoa kwa kutegemea nguvu zetu wenyewe. Ni lazima mioyo yetu imtegemee Mungu kama tukitaka mawazo yetu yawe mema, na kutafakari mambo yale yanayofaa.

Ni wachache wanaotambua kwamba ni wajibu wao kuyatawala mawazo yao pamoja na fikira zao. Ni vigumu kuuweka moyo ambao haujaadibishwa kutafakari mambo yale yaliyo na manufaa. Lakini kama mawazo hayatumiki kama ipasavyo, basi, dini haiwezi kusitawi moyoni.
(RH, Jan. 4, 1881).

Tunapaswa kulifanya Ombi la mtunga Zaburi kuwa ombi letu wenyewe.
"Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako." Zaburi 119:18.

Mara nyingi majaribu yanaonekana yasiyokatilika kwa sababu, kwa njia ya kupuuza maombi na kujifunza Biblia, anayejaribiwa hawezi kukumbuka haraka ahadi za Mungu na kupambana na Shetani kwa kutumia silaha za Maandiko. Lakini malaika wanawazunguka wale wanaopenda kufundishwa katika mambo matakatifu; na hivyo katika wakati wa uhitaji mkuu zile kweli zinazohitajika sana watazikumbuka, kwa hiyo: "Wakati adui atakapoingia kama mafuriko, Roho wa Bwana atainua bendera dhidi yake - Roho wa Bwana atamfukuza." (Pambano Kuu, uk. 497).

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.