
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Mathayo 7:7, 8."
Basi na uje, utafute, na kupata. Ghala la uwezo liko wazi, limejaa na liko huru. Njooni na mioyo yenye unyenyekevu, bila kufikiri kwamba unapaswa kutenda jambo fulani jema ili upate kustahili upendeleo wa Mungu, au kwamba ni lazima ujitengeneze kuwa bora kabla hujaweza kuja kwa Kristo. Kamwe huwezi kufanya jambo lo lote ili kuboresha hali yako. Katika jina la Yesu, njoo ukiwa na uhakikisho kamili wa imani, kwa sababu wewe ni mwenye dhambi; kwa kuwa Kristo alisema, “Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” (Mathayo 9:13). Sogea karibu na Mungu, naye atasogea karibu na wewe. Unapaswa kuomba, kutafuta, kubisha, na kuamini kuwa unakubaliwa kupitia kwa Kristo Yesu, ukimtumainia yeye peke yake kutenda kwa ajili yako mambo yale ambayo kamwe huwezi kujitendea. …
...Yesu ndiye kafara yetu ya upatanisho; hatuwezi kufanya upatanisho wo wote kwa ajili yetu wenyewe, bali kwa imani tunaweza kupokea upatanisho ambao tayari umefanyika. “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu” (1 Petro 3:18). “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, … bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa” (1 Petro 1:18, 19). “Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote” (1 Yohana 1:7). Ni kwa sababu ya damu hii ya thamani roho iliyolemewa na dhambi inaweza kurejeshwa katika uhai. Wakati unapoweka ombi lako kwa Mungu, Roho Mtakatifu anaweka ahadi za Mungu zilizo za uaminifu moyoni mwako.
....Katika nyakati za matatizo, ambapo Shetani anapendekeza mashaka na kukata tamaa, Roho wa Bwana atainua kama bendera dhidi yake maneno ya uaminifu ya Kristo, na miale angavu ya Jua la haki itamulika mara moja katika akili na roho yako. Wakati ambapo Shetani angekushinda kwa kukatisha tamaa, Roho Mtakatifu atakuelekeza katika utetezi uliofanyika kwa ajili yako na Mwokozi aliye hai. Kristo ni manukato, ubani mtakatifu, ambao unafanya maombi yako kukubalika na Baba. Wakati nuru ya haki ya Kristo imefahamika na kupokelewa kikamilifu, upendo, furaha, amani, na shukurani isiyoelezeka vitaenea rohoni, na lugha yake yeye aliyebarikiwa itakuwa “Na unyenyekevu wako umenikuza.” (Zaburi 18:35). - Signs of the Times, Aug. 22, 1892.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon