SAUTI ILIYO WAZI KATI YA SAUTI ZINGINE

Image may contain: text, outdoor and water





Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
Isaya 30:21.

Kati ya machafuko ya mafundisho yanayodanganya, Roho wa Mungu atakuwa kiongozi na ngao kwa wale ambao hawajapinga vithibitisho vya ile kweli. Yeye hunyamazisha kila sauti isipokuwa ile itokayo kwake Yeye aliye Kweli na Uzima. Mungu huwa anampa kila mtu fursa ya kusikia sauti ya Mchungaji wa kweli, kupokea maarifa ya Mungu na Mwokozi wetu. Wakati moyo unapopokea ukweli huu kama hazina ya thamani, Kristo hufanyika ndani, tumaini la utukufu, wakati mbingu yote ikitamka, Amina na Amina! Tunalohitaji dhahiri la nguvu inayoumba upya ya Roho Mtakatifu. Hatuna muda wa kushauriana na damu na nyama.

Tunalo hitaji la nuru ya kimbingu. Kila mtu huwa anapambana kuwa kituo cha mvuto; na mpaka Mungu atakapokuwa amefanyia kazi watu wake, hawataona kuwa kujisalimisha kwa Mungu ni usalama pekee kwa ajili ya roho yoyote. Neema yake inayobadilisha mioyo ya watu itaongoza hadi kwenye umoja ambao bado haujapatikana; kwani wale wote ambao wamechukua mawazo ya Kristo watakuwa katika upatanifu wao kwa wao. Roho Mtakatifu atatengeneza umoja.

“Yeye atanitukuza mimi” (Yohana 16:14) "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3). Roho Mtakatifu anamtukuza Mungu kwa kuifunua tabia yake kwa watu wake kiasi cha kuwa kitu wakipendacho sana na kwa kufanya tabia yake idhihirike ndani yao.

Wanaona wazi kwamba hapangekuwa na uadilifu wowote duniani isipokuwa wake, wala ubora duniani bali ule unaotoka kwake. Roho alipomwagwa kutoka juu, kanisa lilipata mafuriko ya nuru, lakini Kristo alikuwa ndiye chanzo cha ile nuru; jina lake lilikuwa kwenye kila ulimi, upendo wake ulijaza kila moyo. Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati yule malaika atakayeshuka kutoka mbinguni akiwa na uwezo mkuu atakapoangaza dunia yote kwa utukufu wake.

Karama ya Roho wake Mtakatifu, yenye utajiri, iliyojaa, kwa wingi, kwa kanisa lake ni kama ukuta wa moto unaolizingira na nguvu za kuzimu hazitalishinda. Kristo anawaangalia wanafunzi wake katika usafi wao usio na waa wala doa kama zawadi ya kuteseka kwake kote, kudhalilishwa na pia upendo wake, na nyongeza ya utukufu wake – Kristo akiwa kiini kikuu ambapo utukufu wote unatokea. – Home Missionary, Nov. 1, 1893.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.