
Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
1 Petro 3:15.
Hiki ndicho tutakachokiona kama tutaunganika na Mungu. Mungu anataka tumtegemee yeye, sio mwanadamu. Ni shauku yake kwamba tuwe na mioyo mipya; anatupatia ufunuo wa nuru kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Inatupasa tupambane na kila tatizo, lakini wakati suala fulani lililo kinyume linapowasilishwa, utamwendea mtu ili kupata maoni yake na kisha ujenge hitimisho lako kutokana na hayo? La, nenda kwa Mungu. Mwambie unachotaka; chukua Biblia yako na kuchunguza kama atafutaye hazina iliyofichwa.
Huwa hatuingii kwa kina kiasi cha kutosha tunapochunguza ukweli. Kila nafsi inayoamini ukweli wa leo itafikishwa mahali ambapo itahitajika kutoa sababu ya tumaini lililo ndani yake. Watu wa Mungu wataitwa kusimama mbele za wafalme, wakuu, watawala na watu wakubwa wa dunia na ni lazima wajue kwamba wanajua kilicho kweli. Ni lazima wawe wanaume na wanawake walioongoka. Mungu anaweza kukufundisha zaidi katika wakati mmoja kwa Roho wake Mtakatifu kuliko yale ambayo ungeweza kujifunza kutoka kwa wakuu wa dunia hii. Ulimwengu unatazama pambano linaloendelea duniani. Kwa gharama isiyo na kikomo, Mungu amempa kila mtu fursa ya kujua kile kitakachomfanya mtu awe na hekima hadi kufikia wokovu. Malaika wanaangalia kwa shauku ili waone nani atakayejinufaisha na fursa hii!
Ujumbe unapowasilishwa kwa watu wa Mungu,hebu wasiinuke kuupinga; inawapasa waiendee Biblia, wakaulinganishe na sheria na ushuhuda na kama haupiti kwenye mtihani huu, sio wa kweli. Mungu anataka akili zetu zipanuke. Anatamani kutuwekea juu yetu neema yake. Tunaweza kuwa na karamu ya vitu vizuri kila siku; kwani Mungu anaweza kufungua hazina nzima ya mbinguni kwa ajili yetu. Inatupasa kuwa wamoja pamoja na Kristo kama ambavyo yeye ni mmoja pamoja na Baba na Baba atatupenda kama ampendavyo Mwana wake. Tunaweza kuwa na msaada ule ule ambao Kristo alikuwa nao, tunaweza kuwa na nguvu kwa ajili ya kila dharura; kwani Mungu atakuwa mlinzi wetu mbele yetu na nyuma yetu. Selected Messages, vol. 1, uk. 415, 416.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon