MTU MMOJA ALIYESIMAMA

Image may contain: one or more people








Kuna vitu vitatu tu vilivyo vitakatifu katika Biblia, navyo ni NDOA, UBATIZO NA MEZA YA BWANA. Na maandiko matakatifu ndiyo yana ukweli wa wokovu, na ni imani tu iliyo katika Kristo wa Biblia inayoleta WOKOVU. Martin Luther.

Sauti hiyo ilitikisa Ulimwengu wa Katholiki huko Ulaya na kuleta mapinduzi makubwa ya imani. Na kabla ya hapo Martin Luther alipingana na fundisho la INDULGENCE, hilo fundisho ndilo liliipa Roma utajiri mkubwa uliojenga basilica nyingi ikiwemo Basilica kubwa la Vatican city analokaa papa sasa. Indulgence ni malipo ya msamaha wa dhambi ya mateso ya wafu waliokufa katika dhambi huko Pagatori, watu walilipa pesa nyingi sana ili kuokoa ndugu zao waliokufa ambao Roma ilisema wapo katika mateso makali ya moto, na maskofu walitisha waumini mpaka Ulaya ikajaa hofu ya mateso ya kuzimu, ndipo watu walio hai wakamua kujiweka bima ya msamaha wa dhambi, kwa malipo ya pesa, ili wakifa wawe tayari wanamsamaha ulitolewa na Papa. Mungu wa Roma alionekana katili sana. Ndipo siku moja sauti ya matumaini ilisikika, ikipinga na fundisho hilo baya kwa Neno la Mungu, kwamba Mwanadamu anaokolewa kwa imani iliyo katika Kristo, na katika imani hiyo anahesabiwa haki kwa kupokea masamaha ya dhambi, sauti hiyo ni ya kijana machachari Martin Luther. Askofu John Tetzel aliyetumwa na Vatican kukusanya masarafu ya pesa za Wajerumani ya Indulgence alikutana na upinzani mkali sana wa Neno la Mungu na akatoka anazomewa, watu wakaokoka toka katika mikono yake miovu na udanganyifu. Ndipo Roma ikashindwa kuvumilia na kutoa matusi makali sana dhidi ya Martin Luther maana pato lao limepotea.

Matusi ya Papa: Luther ni mwovu, Mbwa na mwana wa Malaya.

Majibu ya Luther: Papa ni Mpinga Kristo na kahaba katika Ulimwengu wa Kikristo.

Msijefikiri nimetunga, lah! Matusi hayo nimenukuu toka katika kitabu kinachoitwa ‘History of Catholic Church, page 105, By Norbert Brockman

Wewe kama mkristo huna sababu ya kuogapa mauti wala kuzimu wala jehanamu, kiasi cha kutoa malipo au kuombea wafu; Yesu anasema hivi:- ‘Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. Yohana 5:24

Leo pia kuna wahubiri wengi ambao wanajitajirisha kwa sadaka za maskini, kwa kutunga mafundisho bandia ambayo si Biblical, kama fundisho la kuuza mafuta ya upako, na mengine yanatoka Nigeria kwa ndege na kuuzwa kwa noti nyingi hapa Tanzania na watu wanazindikia biashara zao na nyumba zao na kazi zao, huo ni uchawi wa kisasa, Chumvi, maji yanauzwa na vitambaa, na mafundisho mengi ya sadaka yanabuniwa, mara sadaka za ukombozi, mara sadaka za wazaliwa wa kwanza, sadaka za baraka za utajiri nk, hao wote wanaofanya hivyo ni watoto wa mpinga Kristo, wanapaswa kukemewa.

Injili haijaweka mzigo huo kwa waumini, NEEMA imetolewa kwa wote; na neema ndiyo nguvu ya injili, ambayo tunaipata kwa imani na si kwa matendo ya sheria au dini. Kwa njia ya imani iliyo katika Kristo, tumepokea haki ya Mungu bure, na mibaraka bure na ulinzi wa Mungu bure.

…wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;….Warumi 3:24

Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani. Wagalatia 3:9

Wafilipi 4:19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Wale wanaokuambia ufanye kitu Fulani ili upate kitu Fulani katika Kristo, hao ni CRIMINAL, Majangili na wanang’anyi, na wahalifu, wanamfanya Kristo kuonekana katili na mtesi wa wenye dhambi, huku yeye alikuja kwajili ya wadhambi na kuwaokoa bure. Hao ni Mafisadi waliokuja katika kanisa kwa siri kubadilisha neema ya Mungu kuwa dili, ‘Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa UFISADI, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Yuda 1:4

Neema ya Mungu ni bure kwa kila aaminiye

Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani. Isaya 55:1
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.