KUANGAZIWA KUPITIA KWA ROHO!

Image may contain: 1 person, ocean, text and water








Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.
Waefeso 1:18.

Mtume Paulo anawasilisha maombi yake kwa Mungu: "Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake” (Waefeso 1:17-19).

Lakini ni lazima mawazo yawe tayari kubadilishwa yawe sawa na tabia ya ile kweli inayochunguzwa. Macho ya ufahamu ni lazima yaangaziwe na moyo na akili viletwe katika upatanifu na Mungu, aliye kweli.Yeye mwonaye Yesu kwa jicho la imani huwa haoni utukufu kwake yeye binafsi; kwani utukufu wa Mkombozi huwa unaakisiwa kwenye akili na moyoni. Upatanisho wa damu yake huonekana na dhambi zinapoondolewa, moyo huamshwa kwa shukurani.



Kristo anapomfanya mtu kuwa mwenye haki, mpokeaji wa ile kweli anashurutishwa kujitoa kikamilifu kwa Mungu na anakubaliwa kwenye shule ya Kristo, ili apate kujifunza kwake yeye aliye mpole na mnyenyekevu wa moyo. Ujuzi wa Mungu unaenezwa kwa upana moyoni mwake. Yeye husema kwa mshangao, Ni upendo wa ajabu! Ni kujishusha kwa ajabu sana! Huku akishikilia ahadi kubwa za imani, mtu huyu anakuwa mshirika wa tabia ya Mungu. Moyo wake ukiwa umeondolewa ubinafsi, maji ya uzima hutiririkia ndani na utukufu wa Bwana hung’aa. Kwa kudumu kumwangalia Yesu, mwanadamu huwa anabadilishwa na Mungu. Muumini anabadilishwa na kufanana na Yesu.

Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo,toka utukufu hata utukufu[toka tabia hadi tabia], kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho” (2 Wakorintho 3:18). Tabia ya mtu hubadilishwa na kuwa ya kimbingu. Ni jicho la kiroho linaloweza kutambua utukufu huu. Huwa unakuwa umetiwa utaji, ukiwa umefunikwa katika fumbo, hadi pale Roho Mtakatifu anapokuwa ameweka utambuzi huu rohoni. – Review and Herald, Feb. 18, 1896.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.