
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia Yohana 5:39.
Kristo alikuja katika umbo la kibinadamu kuiishi sheria ya Mungu. Yeye alikuwa Neno la uzima. Alikuja ili awe injili ya wokovu kwa ulimwengu na kutimiza kila namna ya maelezo bayana ya sheria. Yesu ni neno, mwongozo, ambao lazima upokelewena kutiiwa kwa namna ya pekee kabisa. Ni muhimu sana kuyachunguza machimbo haya ya ukweli na hazina za thamani za ukweli zitagunduliwa na kuhifadhiwa kama madini aghali. Kristo kuwa mtu, Uungu wake, upatanisho wake, maisha yake ya ajabu mbinguni kama wakili wetu, mamlaka ya Roiho Mtakatifu – mada hizi zote za muhimu zilizo hai za Ukristo zinafunuliwa kutoka Mwanzo hadi Ufunuo.Viunganishi hivi vya thamani vya ukweli vinatengeneza mnyororo wa ukweli wa kiinjilisti na wazo kuu la kwanza, linapatikana kwenye mafundisho makuu ya Kristo Yesu. Kwa nini basi, Maandiko haya yasiinuliwe na kutukuzwa kila siku nchini mwetu? Ni namna gani watoto wadogo wanaelekezwa kujifunza Biblia kama Neno la Mungu na kujilisha kwenye ukweli wake, ambao ni mwili na damu ya Mwana wa Mungu!
Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake” (Yohana 6:53–56), “Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa” (1 Yohana 3:24).
Upo umuhimu mkubwa kwa kila familia kuifanya Biblia kuwa kitabu chao cha majifunzo. Misemo ya Kristo ni dhahabu safi, isiyo na uchafu hata kidogo, isipokuwa pale ambapo watu, kwa uelewa wao wa kibinadamu, watajaribu kuiweka mahali fulani, na kufanya uongo uonekane kama sehemu ya ukweli. Wale ambao wamepokea fasiri ya uongo ya Neno, wanapochunguza Maandiko wakiwa na jitihada ya makusudi ya kupata undani halisi wa ukweli uliomo katika hayo, Roho Mtakatifu hufungua macho ya uelewa wao na ukweli wa Neno unakuwa kwao kama ufunuo mpya. – Fundamentals of Christian Education, uk. 385, 386
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon