
"Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake"
1 Yohana 2:4
Lakini Kristo hakuja duniani kuteseka na kufa kwa ajili ya kukamilisha Ukombozi wa wanadamu tu. Alikuja "Kutukuza sheria" na "kuifanya yenye utukufu na heshima." Sio tu kwa wakazi wa dunia hii kuweza kuishika sheria kama inavyopaswa kushika; bali ilikuwa ni kuthibitisha kwa dunia zote za ulimwengu kwamba sheria ya Mungu haibadiliki. Kama madai yake yangekuwa yameondolewa, basi Mwana wa Mungu asingehitajika kutoa maisha yake kufanya upatanisho kwa ajili ya uvunjwaji wake.
Kifo cha Yesu kilithibitisha kutotanguka kwake. Na kwa dhabihu ile ya upendo usio na kipimo uliomsukuma Baba na Mwana kuitoa ili kwamba wenye dhambi waweze kukombolewa, huthibitisha katika ulimwengu wote - si chini ya mpango huu wa upatanisho ambao kingetosha kufanyika - kwamba haki na rehema ndizo msingi wa sheria na serikali ya Mungu.
Katika utekelezaji wa hukumu ya mwisho itaonekana kwamba hakukuwa na sababu ya dhambi kuwepo. Wakati Jaji wa dunia yote atakapomuuliza Shetani "Kwa nini uliniasi, na kunipora raia wa Ufalme wangu?" Mwasisi wa uovu hatakuwa na udhuru. Kila kinywa kitanyamazishwa, na jeshi lote la waasi halitakuwa na cha kusema.
Wakati msalaba wa Kalvari ukiitangaza sheria isiyobadilika, pia huutangazia ulimwengu kwamba mshahara wa dhambi ni mauti.
Katika kilio cha mwisho cha Mwokozi kwamba "Imekwisha", kengele ya Kifo cha Shetani iligonga. Pambano kuu lililokuwa limeendelea kwa muda mrefu hatimaye limekatwa, na ukomeshwaji wa mwisho wa uovu umehakikishwa. Mwana wa Mungu alipitia katika vifungo vya kaburi, ili "Kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi." Waebrania 2:14 Tamaa ya Lusifa ya kujiinua ilikuwa imemsukuma kusema; "Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; ...Nitafanana na Yeye aliye Juu." Mungu alisema: "Nitakufanya kuwa majivu juu ya nchi, ...wala hautakuwepo tena hata milele." Isaya 14:13,14; Ezekieli 28:18. Wakati "siku ile ijayo, ambayo itawaka kama tanuru... Watu wote wenye kiburi, naam, na wote watendao uovu, watakuwa makapi: na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa Majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi." Malaki 4:1.
Ulimwengu wote utakuwa mashahidi wa chimbuko na matokeo ya dhambi. Na uangamizwaji wake ambao mwanzoni ungeweza kuleta hofu kwa malaika na kumdharau Mungu, kwa sasa utathibitisha upendo wake na kudumisha heshima yake kwa ulimwengu wa viumbe ambao hupendezwa kufanya mapenzi yake, na ndani ya mioyo yao kuna sheria yake. Kamwe uovu hautainuka tena. Neno la Mungu linasema: "Mateso hayatainuka mara ya pili." Nahumu 1:9 Sheria ya Mungu ambayo shetani alikuwa ameishutumu kama nira ya utumwa, itaheshimiwa sana kama sheria ya uhuru. Uumbaji uliopimwa na kuhakikiwa kamwe hautaweza tena kugeuza utii kutoka kwake ambaye tabia yake imefunuliwa wazi mbele yao kama yenye upendo wa kina kisichopimika na hekima isiyo na ukomo.
(Pambano Kuu, uk. 417, 418)
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon