
Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
Yeremia 6:16.
Baada ya kumwomba Bwana kwa ajili ya kujua mapenzi yake, kwa ajili ya hekima ya mbinguni, kwa ajili ya nuru ya Roho Mtakatifu, mwombaji atayachunguza Maandiko na kuona kwamba ibara zilizokuwa kama giza akilini mwake mara zimekuwa wazi naye anaelewa wajibu wake kuliko wakati wowote uliopita. Yesu alisema, “Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu” (Yohana 7:16, 17).
Ujuzi wa ukweli wa kimbingu umeahidiwa kwa wale watakaoonesha utii kwa nuru na kwa ukweli ambao wamepewa. Kuingia kupitia kwenye mlango mwembamba hakutegemei kuwa na elimu au utajiri, bali kunategemea hali ya kuwa na roho inayofundishika. Yeye anayethamini mwali wa kwanza wa nuru ya mbinguni na kuitumia, na kutembea katika hiyo, akileta matendo yake katika upatanifu na mwali huo na kutakaswa kupitia kwa huo, atapokea nuru zaidi. Ataelewa kwamba injili ni mpango wa wokovu…
Yeye aliye na moyo wa utii, aliye tayari kufanya mapenzi ya Mungu, hatapokea tu kwa furaha ukweli, bali atautafuta ukweli kwa dhati kama atafutaye hazina iliyofichwa. Atayajia Maandiko akiwa na moyo mnyenyekevu na wenye kufundishika, akitaka kuelewa jinsi awezavyo kutembea nuruni, na akisema, Nifanye nini, Bwana? (Matendo 9:6). Yeye yuko tayari kujinyima chochote na pia kila kitu, kama kitahijika, ili apate kuwa katika upatanifu na mapenzi ya Mungu.
Kuonesha utii kwa mapenzi ya Mungu sio jambo rahisi wakati wote. Kunahitaji uthabiti wa makusudi kuingia kupitia mlango mwembamba na kusafiri kwenye njia nyembamba inayofikisha kwenye uzima wa milele, kwani kila upande kuna sauti zinazoialika nafsi kwenye mambo yasiyo ya muhimu na njia zilizokatazwa. Wale wanaopenda mali na heshima na vyeo vya juu hawataingia kwenye mlango mwembamba wasipoachana na sanamu zao. Hakuna nafasi ya kuingia kupitia kwenye mlango mwembamba huku ukichukua pamoja nawe vitu vya ulimwengu huu.
Yeye atakaye kupitia kwenye mlango mwembaba, ni lazima ajikabidhi kikamilifu na mambo yake yote kwa Mungu. Yesu anasema, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate” (Mathayo 16:24). – Review and Herald, Machi 28, 1912
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon