
"Msiwe na tabia ya kupenda fedha;mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa."
Waebrania 13:5
Ni dhahiri kweli kizazi kipya kinazidi kuwa na nguvu sana miongoni mwetu hasa miaka ya hivi karibuni, wamekuwa na Television zao, radio zao na kumbi mbalimbali kwa ajili ya matamasha yao mbali mbali.
Je umewahi kujiuliza nyuma ya kizazi kipya pamoja na style mbali mbali za uimbaji, mavazi na aina ya maisha waishiyo nani aongozaye????
Leo nitapenda kuongelea aina ya maisha ya kizazi kipya kupitia style mpya ya mtindo wa maisha hasa kwa dada zetu, maana wao ndio wameathirika sana wakitumika kama chombo cha starehe, tutazidi kuyaongea kadri Mungu atupatiavyo pumzi ya uhai.
Mara nyingi tumesikia matangazo mbali mbali yahusuyo aina ya maisha watu wanayopaswa kuishi meengi mwisho utasikia "ISHI KISTAA" Je unajua star wa dunia hii wanavyo ishi??? Dada zetu wamekuwa miongoni mwa waanga wakubwa kwa kujiingiza kwa kujua ama kutokujua katika maisha yasiyo sahihi mbele za Mungu kwa kutamani kuishi maisha ya hali ya juu kuliko uwezo walio nao.
Shetani ameendelea kuwatumia baadhi ya watu kuwavuta wenzao kuingia katika biashara zisizokuwa salama kwa maisha yao kisa tamaa ya pesa, dada wengi wamekuwa wakirubunika kwa aina mbali mbali, wengine udanganywa kutafutiwa kazi nje ya nchi mwisho ujiingiza kwenye madanguro, wengine ufikia mahali ushawishiwa kwa pesa nyingi ili kutengeneza picha za ngono, wengine ucheza uchi (KANGA MOJA) vigodoro, singeli, churaa, pamoja na mambo mengi,......
Shetani anafahamu kuwa muda wake ni mchache sana na anajua hukumu yake iko karibu hivyo anaendelea kubuni njia mbali mbali na namna ya kushikiria akili za watu wasiweze kumtafuta Mungu bali wapumbazwe na mambo ya dunia hii,
"ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."
2 Wakorintho 4:4
moja ya njia Kuu ni pesa na imepelekea kuwavuta kina dada ili wawe shabaha ya kuharibu ndoa za watu kwa kuvaa mavazi mabaya, kujipamba kusiko mpendeza Mungu, miziki ya uchi kuvuta akili za wanaume na kusahau ndoa zao, kisha kuharibu kizazi kizima.
Tangu mwanzo Shetani ameendelea kumtumia mwanamke kama shabaha yake ya kukamata kina baba na kina kaka.
Shetani amekaza hali ya uchumi kuwa ngumu kisha akawafanikisha baadhi (wachache) na kuwaongoza kutumika kuwaharibu wengine, dada wengi urubunika kwa viwango vya pesa na kuuza miili yao, wengine wanadanganyika hata kutengeneza maumbo ya bandia ili waweze kufanikisha kupata pesa kwa njia ya miili yao, wakati huo huo wengine utumika kuwadanganya wakina dada kwa kuwaahidi viwango vikubwa vya pesa kwa ajili ya kujidharirisha mbele ya Jamii kwa kutengeneza picha za ngono, miziki mibaya, uvaaji mbaya mitindo (mamodo) na mambo kama hayo, hata uvaaji wa nusu uchi sasa unaitwa fasheni, tunakwenda wapi??? Lengo kubwa ni kuiingiza Jamii katika dhambi ya ngono.
Ndugu zangu tumefika mwisho sio wakati wa kutumikia dhambi tena, Mungu ameahidi hawezi hakatuacha tufe njaa ikiwa tutamtegemea yeye peke yake.... Mtunga Zaburi anasema:
"Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula."
Zaburi 37:25.
Tunapofanya kazi kwa bidii na kumtegemea Mungu yeye atatufanikisha tuache tamaa na kupenda kuishi maisha ya anasa, hivi karibuni dunia itahukumiwa, muda umekwisha Yesu anarudi andaa maisha yako.
Sheria yake inaendelea kuvunjwa. Miji imechafuliwa na dhambi. Jifunze historia ya Ninawi. Mungu alituma ujumbe maalumu kwa kumtumia Yona kwenda kuhubiri mji huo uliojaa uovu. . . . Ujumbe wa namna hii kama alioutoa Yona utaendelea kutolewa mara nyingi katika kizazi chetu, kama miji hii miovu itatubu kama mji wa Ninawi. - Ms 61 a, June 3, 1906.
Hata katika miji ambapo hukumu za Mungu tayari zimeishaanguka katika matokeo ya uasi huo hakuna dalili ya toba.
Baa na vilabu vya pombe bado viko wazi, na majaribu mengi yanadumishwa mbele za watu. - Letter 268, August 20, 1906.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon