Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao.
Ezra 8:22.
Imani ya Ezra kwamba Mungu angefanya kazi kubwa kwa ajili ya watu wake, ilimwongoza kumwambia Artashasta juu ya hamu yake ya kurudi Yerusalemu kufufua moyo wa kupenda kujifunza neno la Mungu na kusaidia ndugu zake katika kurejesha mji mtakatifu. Ezra alipotamka imani yake kamili katika Mungu wa Israeli kama awezaye kabisa kuwalinda na kuwatunza watu wake, mfalme aliguswa sana…
Alimfanya kuwa mwakilishi maalumu wa ufalme wa Wamedi na Waajemi na akamtunukia mamlaka makubwa kwa ajili ya kukamilisha makusudi yaliyokuwa moyoni mwake…Ndivyo tena watoto waliosambaa walivyopewa fursa ya kurudi kwenye ile nchi wakiwa na vitu vilivyohusianishwa na ahadi kwa nyumba ya Israeli.
Mbele yao ilikuwepo safari ambayo ingechukua miezi kadhaa. Wanaume waliwachukua wake zao na watoto wao na mali zao, kando ya hazina kubwa kwa ajili ya hekalu na huduma yake. Ezra alijua kwamba maadui walikuwa wakivizia njiani, wakiwa tayari kuteka nyara na kumuangamiza yeye pamoja na wote aliokuwa nao; licha ya hivyo, hakumwomba mfalme jeshi lenye silaha kwa ajili ya ulinzi
Katika suala hili, Ezra na wenzake waliona fursa ya kulitukuza jina la Mungu mbele za wapagani. Kuamini nguvu ya Mungu kungeimarishwa zaidi kama Waisraeli wenyewe wangedhihirisha imani yao halisi katika Kiongozi wao wa kimbingu. Kwa hiyo, waliamua kuweka tumaini lao kikamilifu kwake Mungu. Hawakuomba kupewa ulinzi wa askari.
Hawakutaka kumpa mpagani nafasi yoyote ya kupeleka utukufu anaostahili Mungu peke yake kwa nguvu ya mwanadamu. Hawangeweza kuamsha shaka lolote kwa marafiki zao wapagani kuhusiana na ukweli wa tegemeo lao kwa Mungu kama watu wake… Wangeweza tu kulindwa kutokana na kushika na kujitahidi kuitii sheria ya Bwana iliyokuwa mbele yao….. “Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.”
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon