MIJI NI MAHALI PENYE MAOVU MENGI.



Basi jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, Kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu. 
Luka 21:34-36.

Ari ya kupenda anasa na majumba ya starehe kumeshamiri zaidi katika miji. Wazazi wengi wanaochagua makazi ya mijini kwa ajili ya watoto wao, wakidhani kuwanufaisha kwa mengi mengine makubwa, hupambana na majuto, na wakiwa wamechelewa mno ndipo hutubia na kujutia kosa lao baya. Miji ya leo inaharakisha kufanana na Sodoma na Gomora. Siku nyingi za mapumziko hupalilia hali ya kutopenda kazi na uvivu. Michezo ya kusisimua, kwenda kwenye majumba ya starehe ya sinema na maigizo, mashindano ya mbio za farasi, kamari na bahati nasibu, unywaji wa pombe, na starehe zenye makelele - huchochea kila tamaa ya mwili kufanya kazi zaidi. Vijana wanakumbwa na mkondo huu unaopendwa na wengi. - COL 54 (1900).

Nimeonyeshwa nuru kuwa miji itajazwa na machafuko, ghasia na jeuri na makosa ya jinai na kuwa mambo haya yatazidi kuongezeka mpaka mwisho wa historia ya dunia hii. - 7T 84 (1903/2).

Ulimwengu pote, miji inaendelea kuwa mahali penye maovu mengi mabaya. Katika kila upande kunaonekana na kusikika sauti za uovu. Kila mahali kuna vishawishi vya kutimiza tamaa za mwili na ufujaji wa mali. - MH 363 (1905).

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.