ROHO NI WA MUHIMU ILI KUIELEWA KWELI

Image may contain: bird, text and outdoor






Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 1 Kor 2:10.

Ipo kazi kubwa sana ambayo yapasa ifanywe kwa ajili ya wakati huu nasi hatujui hata nusu ya kile ambacho Bwana yuko tayari kukifanya kwa ajili ya watu wake. Tunanena juu ya ujumbe wa malaika wa kwanza na wa malaika wa pili na tunafikiri tunao uelewa wa ujumbe wa malaika wa tatu; lakini haitupasi turidhishwe na ujuzi tulio nao hivi sasa. Maombi yetu, yakichanganyika na imani na toba, vyapasa kupaa kwa Mungu, kwa ajili ya ufahamu wa mafumbo ambayo Mungu atayafanya yafahamike kwa watakatifu wake. Inatupasa tuwe na utambuzi kwamba kama tusipofundishwa na Roho Mtakatifu, hatutaielewa Biblia kwa usahihi; kwani ni kitabu cha Mungu kilichofungwa hata kwa wasomi, ambao ni wenye hekima katika kiburi chao wenyewe.

Yesu alimaanisha alichokisema alipowaelekeza wanafunzi wake “kuyachunguza Maandiko.” Kuchunguza kunamaanisha kulinganisha andiko na andiko, na mambo ya kiroho na yale ya kiroho. Hebu tusiridhishwe na ujuzi wa juu juu. Inatupasa tuchunguze hazina iliyofichwa ambayo imefunikwa isionekane juu, kama mfanyabiashara atafutavyo lulu zilizo nzuri. Nuru, nuru iliyo kuu, itamzawadia mtafutaji mwenye bidii wa ile kweli.

Wapo wengi ambao hawajafanyisha kazi akili zao na ambao hawana uzoefu wa kutumia uwezo wao wote kadiri ya walio nao, katika kujifunza kwamba kweli ni nini. Haiwezekani kwamba Roho Mtakatifu akushukie kama hujisikii kuwa na hitaji, na kama huna shauku sana na ujio wake zaidi ya namna ulivyo sasa. Inakupasa utambue kwamba unaishi kwenye kingo za ulimwengu wa milele, kwamba Kristo anakuja upesi na kwamba mbingu yote inapendezwa na kazi inayoendelea hivi sasa ya kuandaa watu kwa ajili ya ujio wake.

Kama kuna watu waliohitajika kutii mashauri ya Shahidi Mwaminifu kwa kanisa la Laodikia, na kuwa na ari na kutubu mbele za Mungu, ni watu wale ambao ukweli mkuu sana wa wakati huu ulifunguliwa mbele zao na ambao hawajaishi kulingana na fursa za pekee na wajibu wao. Tumepoteza mengi kutokana na kutoishi kulingana na nuru ya ukweli mtakatifu tunaodai kuuamini. – Review and Herald, Juni 4, 1889.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.