NURU HAITOLEWI TOFAUTI NA NENO

Image may contain: outdoor and nature






Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Mathayo 24:24.

Katika siku hizi zilizojaza uongo, kila mmoja ambaye ameimarika katika ukweli itampasa kuitetea imani iliyokabidhiwa kwa watakatifu. Kila namna ya uovu italetwa katika namna ya utendaji wa mafumbo wa Shetani, kwa namna ambayo, kama ingewezekana, ingewadanganya hata wateule na kuwageuzia mbali na ukweli. Kutakuwa na kukutana na hekima ya kibinadamu – hekima ya watu walioelimika, ambao, kama walivyokuwa Mafarisayo, hawa pia ni walimu wa sheria ya Mungu, lakini hawaitii sheria wao wenyewe. Kutakuwa na ujinga wa kibinadamu na upumbavu ambao itapasa ukabiliwe, ambao upo katika nadharia zisizopatana ambazo zimevishwa mavazi mapya na ya kupendeza — nadharia ambazo itakuwa vigumu kukabiliana nazo kwa sababu hazina mantiki ndani yake.

Kutakuwa na ndoto za uongo na njozi zisizo za kweli, ambazo zina ukweli kiasi, bali zinampeleka mtu mbali na imani ya awali. Bwana amewapatia watu kanuni ambayo kwa hiyo wanaweza kuzitambua: “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” (Isaya 8:20). Kama wanahafifisha sheria ya Mungu, kama hawasikilizi mapenzi yake kama yalivyodhihirishwa katika shuhuda za Roho wake, basi ni wadanganyifu. Wanatawaliwa na silika na hisia, ambazo wanaamini zinatoka kwa Roho Mtakatifu na wanadhani kuwa hisia hizo ni za kutegemewa kuliko Neno lililovuviwa. Hawa wanadai kwamba kila wazo na hisia ni mguso wa Roho Mtakatifu; na wanapotoa hoja zenye mantiki kutoka kwenye Maandiko, basi wanatamka kwamba wana kitu kinachofaa kutegemewa zaidi. Lakini hali wakifikiri kwamba wameongozwa na Roho wa Mungu, kwa kweli wanafuata mawazo ambayo yametokana na Shetani. – Selected Messages, vol. 2, uk. 98, 99.

Shetani atafanya kazi kwa namna isiyojulikana kirahisi kuingiza uvumbuzi wa kibinadamu ambao umevikwa mavazi ya malaika. Lakini nuru kutoka kwenye Neno inang’aa kati ya giza la kimaadili; nayo Biblia kamwe haitazidiwa na maonesho ya miujiza. Ni lazima ukweli ujifunzwe, ni lazima utafutwe kama hazina iliyojificha. Nuru za ajabu hazitatolewa pembeni ya Neno, au kuchukua nafasi yake. Ng’ang’ania Neno, pokea Neno lililowekwa moyoni, ambalo litafanya watu wawe na hekima ifikishayo wokovuni. – Ibid., uk. 100.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.