NAMNA ROHO ANAVYOTUONGOZA


No automatic alt text available.




Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
Yohana 10:27.

Yesu anategemea kwamba wale wote wanaodai kuwa askari wake watumike kwa ajili yake. Yesu anakutarajia wewe umtambue adui na kumpinga, siyo kumleta karibu na ujasiri wako na kwa namna hiyo kusaliti amana takatifu. Bwana amekuweka mahali ambapo utainuliwa na kuadilishwa na utadumu kuendelea katika kupata hali ya kufaa kwa ajili ya kazi yake. Kama hutapata sifa hizi; wewe mwenyewe utakuwa ndiwe wa kulaumiwa.

Zipo njia tatu ambazo kwazo Bwana huwa anadhihirisha mapenzi yake kwetu, kutuongoza, na kutufanya tufae kuongoza wengine. Tunawezaje kuitofautisha sauti yake na sauti nyingine ngeni? Tunawezaje kuitofautisha na sauti ya mchungaji mwongo? Mungu anadhihirisha mapenzi yake kwetu katika Neno lake, Maandiko Matakatifu. Sauti yake huwa inadhihirika katika kazi zake za kimbingu; nayo itatambulika nafsini mwetu ikiwa hatutajitenga na Yeye kwa kwenda katika njia zetu wenyewe, tukitenda kulingana na nia zetu wenyewe na kufuata ushawishi wa moyo ambao haujatakaswa, hadi hisia zitakapokuwa zimechanganyikiwa kiasi cha mambo ya milele kutotambuliwa na sauti ya Shetani kugeuzwa kwa hila kiasi cha kukubalika kama sauti ya Mungu.

Njia nyingine ambayo kwayo sauti ya Mungu husikika ni kupitia kwa miito ya Roho wake Mtakatifu, akiweka miguso moyoni, ambayo itaonekana kwenye tabia. Kama una mashaka kuhusu somo lolote, lazima kwanza uangalie Maandiko. Kama kweli umeanza maisha ya imani, unakuwa umejitoa mwenyewe kwa Bwana kuwa wake kikamilifu, naye amekuchukua ili akuumbe na kukutengeneza kulingana na kusudi lake, ili upate kuwa chombo cha heshima. Inakupasa uwe na shauku ya dhati ya kuwa mwepesi kubadilishwa mikononi mwake na kumfuata popote anapokuongoza. Ndipo utakuwa ukimtegemea kutekeleza mipango yake, wakati huo huo ukishirikiana naye kwa kutimiza wokovu wako wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Wewe ndugu yangu, utaona vigumu hapa kwa sababu hujajifunza kwa uzoefu kujua sauti ya Mchungaji Mwema na hili linakuweka katika mashaka na hatari. Yakupasa uweze kuitambua sauti yake. – Testimonies, vol. 5, uk. 511, 512.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.