MATENGENEZO YA AFYA KUAMBATANA NA UJUMBE WA MALAIKA WA TATU

Image may contain: cloud, sky and text







"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo"
3 Yohana 1:2

"Kuiweka wazi sheria ya asili, na kusisitiza utii kwayo, hii ndiyo kazi inayoambatana na ujumbe wa Malaika wa tatu ili kuwatayarisha watu kwa marejeo yake Bwana."
(Testimonies, vol 3, uk. 161).

Kusudi la matengenezo ya afya (Health reform) ni kuusafisha Ubungo ili uweze kuipambanua kweli na kuuweka mwili katika hali ifaayo sana kutenda kazi ya Mungu.

"Yeye (Mungu) ameazimu kwamba somo hili (la matengenezo ya afya) litahubiriwa kwa mapana yake na mioyo ya watu itaamshwa kwa kina ili kulichunguza; kwa maana haiwezekani kwa wanaume na wanawake, wakiwa chini ya nguvu za mazoea ya dhambi, yaharibuyo afya, na kuudhoofisha ubongo, kuweza kuithamini kweli hii takatifu."
(Maranatha, uk. 119).

"Mungu anawataka wote wanaoiamini kweli kufanya juhudi thabiti, zinazoendelea daima kwa kujiweka wenyewe katika hali bora sana ya afya ya mwili wao, kwa kuwa kazi nzito sana na ya muhimu iko mbele yetu. Afya ya mwili na Roho inatakiwa kwa kazi hii; ni ya muhimu kwa maisha ya kidini yenye afya... kama ulivyo mkono au mguu kwa mwili wa mwanadamu."
(Testimonies, vol 1, uk. 619).

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.