
Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu.
1 Wakorintho 2:4.
Nimeona ya kwamba hatari ipo katika kila hatua ya uzoefu wa kanisa, kwa sababu wapo wanaosikiliza mambo wakiwa na nia mbaya. Wakati baadhi ya walimu wakiwa na nguvu na ufanisi katika kufundisha kulingana na mafundisho ya Biblia, sio wote wakataokuwa watu wenye ujuzi wa maisha halisi ya vitendo na wanaoweza kushauri akili zenye fadhaa kwa uhakika na usalama. Hawa hawaoni hali inayotatiza ambayo ni muhimu iifikie kila familia itakayofanya mabadiliko. Kwa hiyo, hebu wote wawe waangalifu kwa kile wakisemacho; kama hawajui mawazo ya Mungu katika masuala fulani, hebu kamwe wasiseme kutokana na kukisia au kudhania. Kama hawajui lolote kwa namna iliyo wazi, hebu waliseme hilo na hebu mtu mmoja binafsi amtegemee Mungu kikamilifu. Hebu pawe na kuomba kwingi na hata pamoja na kufunga, kwamba pasiwepo na hata mmoja atakayetenda gizani, bali atatenda katika nuru kama Mungu alivyo katika nuru.
Tunaweza kutafuta chochote ili tuonekane nje na ndani ya kundi letu; na zipo akili ambazo hazijanidhamishwa na neema ya Roho Mtakatifu, ambazo hazijatenda maneno ya Kristo na ambazo hazielewi utendaji wa Roho wa Mungu, ambao watakwenda katika njia mbaya ya utendaji kwa sababu hawamfuati Yesu kikamilifu. Hawa wanakwenda kulingana na hisia na mawazo yao wenyewe.
Hebu pasifanyike chochote kwa namna isiyo katika utaratibu, ambayo inaweza kusababisha hasara au kujinyima vitu kwa sababu ya hotuba motomoto za hisia, ambazo zinaamsha msisimko usiopelekana na utaratibu wa Mungu, kwamba ushindi ambao ulikuwa ni muhimu upatikane, utageuka kuwa kushindwa kutokana na kutokuwa na kiasi katika utulivu na kutafakari kwa usahihi na kanuni na makusudi mazuri. Hebu uwepo na uongozi wenye hekima katika hili na wote waende chini ya uongozi wa Mshauri asiyeonekana, mwenye hekima, ambaye ni Mungu. Vile vilivyo vya kibinadamu vitapambana kwa ajili ya kutawala mambo na hata inawezekana kukawa na kazi itakayofanywa ambayo haitakuwa na sahihi ya Mungu. – Special Testimonies Relating to Various Matters in Battle Creek, uk. 17, 18.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon