KUKUZA UTAMBUZl WA KIROHO


Image may contain: ocean and text








Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 1Wakorintho 2:14.

Vito vya ukweli vimeenea kwenye shamba la ufunuo; lakini vinakuwa vimezikwa chini ya mapokeo ya kibinadamu, chini ya misemo na amri za watu. Hekima kutoka mbinguni imepuuziwa katika matendo; kwani Shetani amefanikiwa kuufanya ulimwengu kuamini kwamba maneno na mafanikio ya watu ndiyo ya muhimu sana. Bwana Mungu, Muumba wa ulimwengu, ameupatia ulimwengu injili kwa gharama ya juu isiyo na kikomo. Kupitia kwa huyu wakala wa kimbingu, chemchemi za furaha zinazohuisha za amani ya mbinguni na faraja inayodumu vimefunguliwa kwa wale watakaijia chemchemi ya uhai. Kuna vena za ukweli ambazo bado hazijagunduliwa; lakini mambo ya kiroho yanatambulika kwa jinsi ya rohoni.

Mioyo iliyozingwa kwa uovu haiwezi kutambua thamani ya ukweli kama ulivyo katika Yesu. Uovu unapolelewa, watu hawajisikii kufanya jitihada ya dhati kwa maombi na kutafakari, kuelewa kwamba ni lazima waijue au waipoteze mbingu. Kwa muda mrefu wamekuwa chini ya kivuli cha adui kiasi kwamba wanaona ukweli kama watu waonao vitu kupitia kwenye kioo chenye moshi au kisicho katika hali nzuri; kwani kwao, mambo yote yanakuwa ni giza na upotovu machoni pao. Uwezo wao wa kiroho wa kuona ni dhaifu na usioaminika; kwani wanatazama kivuli na kuipa nuru mgongo.

Lakini wale wanaodai kumwamini Yesu yapasa wadumu katika nuru. Inapasa waombe kila siku kwa ajili ya nuru ya Roho Mtakatifu ili awaangazie kurasa za kitabu kitakatifu, ili wawezeshwe kuelewa mambo ya Roho wa Mungu. Ni lazima tuwe na tumaini lisiloyumba katika Neno la Mungu, vinginevyo tutapotea. Maneno ya watu, hata wawe wakubwa kiasi gani, hayawezi kutufanya tuwe wakamilifu, kutufanya tukamilishwe kutenda kila tendo jema.

Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli’ (2 Wathesalonike 2:13). Kwenye aya hii, mawakala wawili katika wokovu wa mwanadamu wamedhihirishwa – mvuto wa kimbingu, ulio na nguvu, imani iliyo hai ya wale wanaomfuata Kristo. Tunakuwa watendakazi pamoja na Mungu kupitia kwa utakaso wa Roho na kuiamini kweli. – Review and Herald, Dec. 1, 1891.



”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.